Wednesday , 1 May 2024
Home Kitengo Biashara Miaka 20 iliyopita luninga ilikuwa ni ishara ya utajiri
Biashara

Miaka 20 iliyopita luninga ilikuwa ni ishara ya utajiri

Mtendaji Mkuu wa Samsung Electronics Tanzania, Manish Jangra
Spread the love

 

UKINIULIZA nikutajie idadi ya vifaa vya umeme mashuhuri vilivyokuwa vinatumiwa na Watanzania wengi nyumbani kwa kipindi cha miongo miwili iliyopita nitakujibu kuwa ni luninga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Najua unaweza kustaajabu lakini ndio uhalisia kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na hali ilivyo sasa ambapo karibu kila shughuli ya nyumbani inafanywa na kifaa cha umeme.

Ukimuuliza mtu yoyote kwa kipindi kile kwanini usinunue jiko, birika la umeme, jokofu, mashine ya kufulia, mashine ya kusagia matunda na viungo vya kupikia, au air condition, atakujibu kuwa ni anasa kuwa navyo na vinaongeza matumizi ya umeme hivyo gharama za Maisha.

Lakini hali imebadilika kwa kiasi kikubwa sasa, watu wengi wanafikiria mbinu tofauti za kurahisisha Maisha yao ya kila siku, yaani kufanya vitu vingi ndani ya muda mfupi.

Kwa mujibu wa Statista, Mnamo 2024, mapato katika soko la vifaa vya nyumbani nchini Tanzania yanafikia Dola za Marekani bilioni 3.03. Soko hili linakadiriwa kukua kila mwaka kwa asilimia 5.54 (CAGR 2024-2028).

Kufikia 2024, mauzo ya mtandaoni yanatarajiwa kuchangia asilimia 1.1 ya mapato yote katika soko la vifaa vya nyumbani nchini Tanzania. Kwa kuongezea, soko la vifaa vya nyumbani linatarajiwa kupata ukuaji wa asilimia 3.9 mnamo 2025.

Hii ni ishara nzuri kwa ukuaji na ongezeko la matumizi ya vifaa vya nyumbani ambapo kwa miaka mingi makampuni ya utengenezaji na usambazaji wa vifaa vya umeme kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani yamekuwa yakihamasisha.

Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokuwa kwa kasi barani, matumizi sahihi ya muda wa uzalishaji ni suala ambalo halihitaji mjadala kwa sasa.

Ni kawaida kwa sasa kukuta familia nyingi za Kitanzania hazitumii tena mkaa na kupoteza muda kuandaa kifungua kinywa. Uwepo wa vifaa kama mabirika na majiko ya umeme vimerahisisha na kuokoa muda ambao ulikuwa unapotezwa asubuhi. Kwa mfano, miaka kadhaa nyuma ilibidi mama au dada wa kazi aamke asubuhi na mepema ili kuwaandalia Watoto kifungua kinywa kabla ya kwenda shule. Lakini kwa sasa, humhitaji kama dakika 10 tu kwasababu vifaa vya kumrahisishia vipo.

Pia, nakumbuka miaka ya nyuma ambapo ilikuwa inawachukua watu siku nzima kufua nguo, tena usiombe kama una familia kubwa, zoezi linaweza kuchukua hata siku mbili kama sio kuahirishwa mpaka wiki ijayo. Yalikuwa ni mateso kwa akina mama au dada wa kazi kwasababu licha ya kupoteza siku nzima, lakini zoezi hilo huwaacha na uchovu usioelezeka wakati kazi nyingine za nyumbani zikiwasubiria.

Ufuaji wa nguo kwa sasa umerahisisha kutokana na kuwepo kwa mashine za kisasa ambazo zina uwezo mkubwa na rahisi kutumia. Mtu anajiandaa kabisa kwa ufuaji kwa kufanya maandalizi machache bila ya kuuchosha mwili na kupata muda wa kufanya shughuli zingine.

Kwa ufupi, vifaa vya nyumbani vimekuja na faida ya kufanya shughuli nyingi kwa urahisi, haraka na kutupatia muda wa kufurahia matukio mengine ambayo yasingewezekana kufanyika kwa pamoja. Kwa mfano, ilikuwa ni vigumu kwa miaka ya nyuma siku ya kufanya usafi nyumbani ukapatikana na muda wa kwenda kutembea na kufurahia na familia yako.

Maendeleo haya kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na ongezeko la ueneaji na matumizi ya umeme nchini.

Kwa mujibu wa ripoti ya Tathmini ya Soko la Kupika iliyofanywa na taasisi ya Modern Energy Cooking Services (MECS) ya mwaka 2022, kwa miaka ya hivi karibuni Tanzania imepata maendeleo makubwa katika usambazaji wa umeme kwa zaidi ya mara mbili kati ya 2010 na 2020 kutoka 15% hadi 40% (Benki ya Dunia, 2022a).

Serikali ina mipango kabambe ya upanuzi wa upatikanaji wa umeme na kuongeza uwezo wa uzalishaji, ikilenga karibu MW 6000 kuongezeka ifikapo mwaka 2026, asilimia 65 kati ya hizo zitatokana na vyanzo mbadala (Wizara ya Fedha na Mipango, 2021).

Kwa jitihada hizi, hofu ambayo wateja wengi wanayo kwa miaka mingine haitokuwa changamoto tena kwasababu ongezeko la uzalishaji na usambazaji wa umeme litaenda sambamba na kushuka kwa gharama. Hivyo, hata manunuzi na matumizi ya vifaa vya nyumbani yataongezeka zaidi na kufikia Watanzania wengi nchini kote.

Unapozungumzia matumizi ya vifaa vya umeme vya nyumbani bila shaka utayajumuisha na teknolojia za kisasa kama vile usimamizi uliorahisishwa kwa vifaa vinavyotumia intaneti kama vile simu za mkononi.

Wazalishaji na wasambazaji wa vifaa vya nyumbani wamefikiria mbali zaidi katika kumrahisishia mtu shughuli za kila siku. Kwa mfano, kutokana na kuwa na mambo mengi ukasahau kuzima vifaa vyako nyumbani utafanyaje? Lakini kwa teknolojia kama 3D Map View iliyozinduliwa na kampuni ya Samsung Electronics, sasa unaweza kuona kwa uhalisia vifaa vyako vya nyumbani na kusimamia matumizi yake ukiwa mbali bila ya wasiwasi.

Kama wewe ni miongoni wa wale wanaogopa kuwa na vifaa vingi vya umeme kwa matumizi ya umeme ukiona ni anasa, nakuomba uachane na huo mtazamo wa kizamani.

Hebu fikiria urahisi na muda utakaokuwa unauokoa kila siku kwa kufanya maandalizi machache na kufanya mambo mengine ambayo unadhani hayawezekani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Biashara

Wazir Jr kinara wa ufungaji KMC FC ajiunga Meridianbet

Spread the love    MUITE Wazir Jr ‘The King of CCM Kirumba’,...

Biashara

Meridianbet Expanse Tournament ushindi rahisi  

Spread the love  Jisajili na Meridianbet kisha uwe wa kwanza kupata taarifa...

Biashara

Mbinu bora za kubeti kwa mafanikio

Spread the love  MIONGONI mwa burudani zinazidi kupata umaarufu ulimwenguni, kubeti katika...

error: Content is protected !!