Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mtoto aliyesaidiwa matibabu na Rais Samia atoa simulizi ya kusisimua
Habari Mchanganyiko

Mtoto aliyesaidiwa matibabu na Rais Samia atoa simulizi ya kusisimua

Spread the love

 

KIJANA Hamimu Mustapha Baranyikwa (15), mkazi wa kijiji cha Nyakanazi, Biharamulo, Mkoani Kagera, amesimulia jinsi alivyougua maradhi ya ngozi mwilini mwake kwa muda mrefu kabla ya kupata msaada asioutarajia kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati alipofanya ziara mkoani humo tarehe 16 Oktoba, 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mara kwa mara Rais Samia anapokuwa ziarani sehemu mbali mbali hapa Tanzania hukutana na watu wakamwelezea shida zao binafasi na akazipatia ufumbuzi.

Lakini tukio moja la Oktoba 2022 lilikuwa la aina yake na limebadili maisha ya mtoto mmoja.

Katika msafara wake akiwa ziarani mkoani Kagera, Rais Samia alimkuta mtoto wa kiume Hamimu Baranyikwa akiwa amekaa pembezoni mwa barabara akionekana kuwa na huzuni kubwa.

Ngozi ya mtoto huyu mwili mzima ilikuwa imeharibika vibaya kwa maradhi.

“Watu walikua wananiogopa, nilikua sichezi na watoto wenzangu. Hata watu wazima walikua wakiniona tu wananikimbia,” alisema Hamimu.

“Niliteseka kwa waganga, hadi nikasema mniache tu nife. Nilikosa amani, nikawa nakaa tu ndani. Sitoki nje.”

Rais Samia aliguswa na hali ya mtoto huyo na kuagiza wasaidizi wake wamfuate na kumdadisi zaidi.

Baada ya kupata maelezo yake, Rais aliagiza mtoto huyo apelekwe Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kufanyiwa uchunguzi, kabla kuanza kutibiwa chini ya udhamini wake mwenyewe Rais Samia.

Habari njema ni kwamba, takriban miezi sita tangu Hamimu aanze kutibiwa, amepata nafuu ya hali ya juu.

Hamimu sasa ameruhusiwa kutoka hospitalini kwenda nyumbani Aprili 19, 2023.

“Sasa naweza kushika vitu na mkono na hata kula ugali na sura yangu inaonekana,” alisema Hamimu akiwa hospitali ya Muhimbili baada ya matibabu.

Hamimu alipokelewa na kuanza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tarehe 21 Oktoba, 2022 kwa msaada wa Rais Samia.

Na sasa ameruhusuiwa kurejea nyumbani kwa wazazi wake Nyakanazi Mkoani Kagera baada ya hali yake kuimarika na amemshukuru Rais Samia kwa moyo wake wa kumsaidia na kuokoa maisha yake.

“Tumehangaika hapa na pale hadi imeshindikana yeye akaniona. Huku kwetu kuna watu wenye hela lakini wameshindwa kunisaidia,” alisema.

“Namshukuru Mama Samia. Ingekuwa inawezekana, nilikua natamani nimuone hivi kwa macho kwa jinsi alivyonisaidia.”

1 Comment

  • VIONGOZI WANAOONGOZA KUKOSOA MAAMUZI YA VIONGOZI WENZAO TANZANIA….. KWA MBINU ZOTE TULIZANI HUWA MANAKUBALIANA
    Mwanasiasa maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche ametema cheche kuhusu sakata linaloendelea la Kampuni ya Twiga Cement kutaka kuinunua Kampuni ya Tanga Cement.

    Her Excel. Samia Suluhu

    Mr. Daniel Chongolo

    Mr. Professor Ibrahim Haruna

    Mr. Hamad Masoud Hamad

    Mr. Freeman Aikael Mbowe

    Mr. John John Mnyika

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!