Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mrema afariki dunia
Habari MchanganyikoTangulizi

Mrema afariki dunia

Spread the love

MWENYEKITI wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki duninia leo tarehe 21 Agosti, 2022, saa 12.15 asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ofisa Habari Mwandamizi wa MNH, Aminieli Eligaisha amethibitisha na kuongeza kuwa Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia tarehe 16 Agosti,2022 na kufikwa na mauti leo asubuhi.

Mrema aliyewahi kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani, alizaliwa Desemba 31, 1944, katika kijiji cha Kiraracha- Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 mwanasiasa huyo alimgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pia Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na umauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!