Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mjema ‘out’ CCM, Makonda atajwa
Habari za SiasaTangulizi

Mjema ‘out’ CCM, Makonda atajwa

Spread the love

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Sophia Mjema kuwa Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na Makundi Maalum.

Kabla ya uteuzi huu Sophia alikuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mwanamama huyo anaweka rekodi ya kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi aliyeshika nafasi hiyo kwa muda mfupi wa miezi tisa na ushee.

Hata hivyo, kabla ya uteuzi wa sasa, Sophia aliibua mijadala kwa wachambuzi wa masuala ya kisiasa baada kudai kwamba Rais Samia anapaswa kuiongoza Tanzania kwa miaka 10 ijayo kuanzoa mwaka 2025.

Mjema alitoa kauli hiyo mkoani Mara wakati akizungumza na wanawake mkoani humo ambapo alisema kwa utendaji na kasi anayoionesha Rais Samia anastahili miaka 10 kuanzia mwaka 2025.

Mbali na kupingwa vikali kuwa ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayomtaka Rais kuongoza kwa mihula miwili, tayari wengi wao walikuwa wamebainisha kuwa nafasi hiyo ya kisiasa ndani ya CCM haimtoshi.

Hayo yanajiri wakati CCM ikijipanga kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.

Hata hivyo, kutokana na joto hilo la uchaguzi fununu za Sophia kung’olewa kwenye nafasi hiyo zilianza mapema wiki hii baada ya Rais Samia kuitisha Mkutano wa dharura wq halmashauri kuu ya taifa CCM (NEC) huku aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitajwa kupeww nafasi ya Sophia.

Makonda ambaye ni mmoja wa wanasiasa machachari ameibua mjadala ndani ya mitandao ya kijamii kutokana na aina ya siasa za mapambano amekuwa akizifanya dhidi ya wapinzani wake ndani na nje ya CCM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!