Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mhasibu Serengeti aswekwa rumande kwa madai ya kutafuna mil. 214
Habari za SiasaTangulizi

Mhasibu Serengeti aswekwa rumande kwa madai ya kutafuna mil. 214

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Spread the love

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, ACP Salum Morcase amkamate Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Saad Mutunzi Ishabailu kwa kosa la kuhamisha Sh. 214 kwa awamu nne. Anaripoti Mwandishi Wetu … ( endelea).

Amedai Mhasibu huyo amehamisha fedha hizo kwa njia ya uhamisho wa ndani kwa kushirikiana na watumishi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi.

“Mkamate huyo bwana sasa hivi aende polisi akafunguliwe mashtaka, huyu ni wa kupeleka mahakamani moja kwa moja. DPP aelezwe afungue jalada la mashtaka.

“Wale wenzake tumewapeleka mahakamani tayari sababu tulibaini walihusika na wizi kama huu kwenye Manispaa ya Kigoma mwaka jana,” ameagiza Majaliwa.

Ametoa agizo hilo leo Jumanne jioni wakati akizungumza na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwenye kikao kilichofanyika katika kwenye Halmashauri hiyo, mkoani Mara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!