Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mambo 3 yateka mdahalo wagombea ngome vijana ACT-Wazalendo
Habari za SiasaTangulizi

Mambo 3 yateka mdahalo wagombea ngome vijana ACT-Wazalendo

Spread the love

WAGOMBEA Uenyekiti wa Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, wamenadi sera zao katika mdahalo wa uchaguzi, wakiwaomba wajumbe wawachague kwenye uchaguzi utakaofanyika Alhamisi ya tarehe 29 Februari mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mdahalo huo umefanyika leo Jumanne, tarehe 27 Februari 2024, huku matatizo ya vijana wa kitanzania, ukata wa fedha ndani ya ngome hiyo na kukosekana kwa ushirikiano kuanzia ngazi ya taifa hadi chini, vikiteka mdahalo huo.

Wagombea katika kinyang’anyiro hicho ni, Ruqayya Nassir, Mhandisi Ndolezi Petro, Abdul Nondo na Julius Massabo.

Akizungumza katika mdahalo, Ruqayya ametaja vipaumbele vyake vinne, ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa, kulinda maslahi ya vijana na kutafuta vyanzo vya mapato vya uhakika vya ngome hiyo.

“Tunataka kuimarisha mfumo wa uongozi ndani ya ngome yetu na isiwe tu uongozi uko taifa tunataka uongozi uliokamilika kuanzia taifa mpaka ngazi ya tawi.

“Mwenyekiti amekiri changamoto kubwa ambayo ngome ilipitia ni uhaba wa fedha, nikiingia nitahakikisha nabuni vyanzo vya mapato vya kuaminika na kupata fedha ili kupata uhuru kufanya program za ngome,” amesema Ruqayya.

Massabo ametaja vipaumbele vyake vinne ikiwemo kuwaunganisha vijana na kubuni vyanzo vipya vya mapato.

“Tunaongozwa na vipaumbele vikubwa sita na tuna matumaini ndani ya miaka mitano endapo tutachaguliwa tutakuwa tumeshakamilisha. Vipaumbele vyetu itakuwa tuna wajibu wa kuijenga ngome kitaasisi ngome ya vijana sio tu taifa, tunataka kuwa na ngome kwenye mikoa, taifa na majimbo. Kipaumbele kingine kuwapatia vijana wageni mafunzo waweze kusimama na kukisemea chama chao,” amesema Massabo na kuongeza:

“Pia, ngome imekuwa na changamoto ya mapato mwenyekiti anayemaliza muda wake ameeleza kuna changamoto ya fedha sisi tutafanya tofauti hatutaridhika fedha inazopata ngome tutatafuta vyanzo vipya.”

Naye Mhandisi Ndolezi amewataka wajumbe hao wamchague ili aiimarishe ngome hiyo na ACT-Wazalendo, kwa kuwa ana uzoefu wa kufanya operesheni za chama hicho nchi nzima.

“Kwa muda wote nimekuwa mtumishi wa hiki chama kwa uaminifu mkubwa, nimefanya operesheni nyingi ndani ya nchi takribani majimbo 264 tumemaliza kuzunguka tukifanya ujenzi wa chama, nilishiriki utekelezaji wa mfumo wa kidigitali wa ACT- Wazalendo Kiganjani, miongoni mwa vijana tulioshiriki kusimamia chaguzi za majimbo na mikoa kitu kilichopelekea kupata viongozi wa chama nchi nzima,” amesema Mhandisi Ndolezi.

Aidha, Ndolezi ametaja vipaumbele vyake ikiwemo kuwaunganisha vijana wa ACT-Wazalendo na watanzania kwa ujumla, kufanya ngome hiyo kuwa kimbilio la utatuzi wa matatizo ya vijana, kutafuta vyanzo vya mapato kwa ajili ya kupata fedha za kuendesha program za ngome hiyo.

Kwa upande wake Nondo, amewataka wajumbe wa ngome hiyo wamchague tena ili akamilishe yale ambayo aliahidi kutekeleza katika awamu yake ya kwanza ya uongozi.

“Vipaumbele vyetu sasa ambavyo hatukuvifanya kwa ufanisi kama tulivyotaka na ndio maana tunaomba ridhaa kwenu tuyakamilishe. Kwanza kuwajengea uwezo na kutoa mafunzo kwa vijana, kutanua wigo wa vyanzo vya mapato,”

“Kuendelea kutetea maslahi na madai ya vijana kwa serikali na vikao vya chama. kuimarisha mtandao wa chama nchi nzima, kutanua na kuimarisha mtandao wa matawi ya ACT-Wazalendo na kuhamasisha vijana kugombea na kulinda ushindi kwenye uchaguzi wa 2024 na 2025,” amesema Nondo.

Nondo ametaja mambo mbalimbali aliyofanya pamoja na wenzake, ikiwemo kuimarisha ngome hiyo.

“Tumeingia 2020 ngome haina fedha, tumefanya kazi 2020 yote hakuna hela, 2021 yote hakuna hela, 2022 ndio tumeanza kupokea ruzuku kutoka chama Sh. 300,000 kwa mwezi lakini tulifanya kazi katika wakati mgumu,” amesema Nondo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!