Saturday , 2 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Mfanyabiashara Tanga amwangukia Majaliwa zabuni ya Jamhuri Pack ‘Forodhani’
Habari Mchanganyiko

Mfanyabiashara Tanga amwangukia Majaliwa zabuni ya Jamhuri Pack ‘Forodhani’

Mfanyabiashara, Sultan Salim
Spread the love

 

MFANYABIASHARA Sultan Salim wa jijini Tanga, amemuomba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Kassim Majaliwa, kuingilia kati mchakato wa upatikanaji wa mshindi wa zabuni wa eneo la Jamhuri Pack ‘Forodhani’ jijini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imekuja baada ya mfanyabiashara huyo kudai kudhulumiwa haki yake kutokana na mchakato ulivyofanywa hadi kupatikana mshindi kuna taratibu na kanuni zimekiukwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Salim alisema kinachoonekana wanataka kumnyima haki yake kwa makusudi kwani alistahili kushinda tenda hiyo kutokana na dau kubwa alilotoa.

“Agosti Mosi, mwaka huu niliomba tenda hiyo ya Jamhuri Pack na nashukuru nilishinda kwakuwa dau langu la sh. milioni 2 na mia mbili hakuna ambaye alilifikia siku hiyo ya ufunguzi wa zabuni hiyo,” alisema na kuongeza;

“Lakini chakushangaza Halmashauri ya Jiji la Tanga ilivyofika Agosti 8, mwaka huu wakatoa makusudio ya upangaji na kumtangaza Ali Salim Mohamed kuwa mshindi kwa dau la sh. mil. 2.3 wakati siku ya ufunguzi tenda hiyo alitoa dau la Sh. 1.3 milioni.”

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu,

Alisema anashangaa kuona mpinzani wake kutangazwa ameshinda tenda hiyo wakati siku ya ufunguzi alitoa dau dogo na yeye alitoa kubwa kitu ambacho kinampa maswali mengi bila majibu.

Akifafanua zaidi alisema baada ya sintofahamu hiyo aliandika barua kwenda halmashauri kupinga matokeo hayo pamoja na kuweka zuio lakini majibu yakabaki vile vile.

“Halmashauri ilijibu kwa kutilia mkazo matokeo yao ya awali waliyoyatoa na hata nilipoandika barua ya pili kwao na kuambatanisha na nyaraka zote za mchakato mzima ulivyoanza hadi kunionesha mimi ndiye nilipaswa kuwa mshindi, haikusaidia kitu kwani halmashauri ilikataa kupitia nyaraka zangu,” alisema Salim.

Alisema kutokana na sintofahamu hiyo ndio maana ameamua kukimbilia kwa Waziri Mkuu, Majaliwa akiamini atalifanyia kazi na ukweli kuwekwa wazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

Habari Mchanganyiko

Heche ataka mawakili vijana kuamka sakata Mpoki

Spread the loveMWENYEKITI wa Mawakili Vijana Tanzania kutoka Chama cha Mawakili wa...

error: Content is protected !!