Saturday , 2 December 2023
Home Habari Mchanganyiko DED Momba apongezwa kwa kufikia 54% ya mapato kabla ya muda
Habari Mchanganyiko

DED Momba apongezwa kwa kufikia 54% ya mapato kabla ya muda

Mkurugenzi Mtendaji wa Momba, Regina Bieda
Spread the love

 

KATIBU tawala mkoani Songwe, Happiness Seneda, ameupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Momba kwa kufikisha asilimia 54 ya makusanyo ya fedha. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea).

Seneda aliyasema hayo le tare 14 Novemba, 2023 wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo ambapo licha ya kukagua miradi mbalimbali pia alitumia nafasi hiyo kuipongeza halmashauri hiyo kwa kufikisha asilimia 54 ukilinganisha na halmashauri zingine.

“Nipo wilayani Momba kukagua miradi nikianzia wilayani Mbozi, miradi ipo vizuri, kasoro zilizopo zirekebisheni, nikupongeze mkurugenzi na timu yako mpo vizuri endeleeni na ushirikiano huo ili msonge mbele “ameema Ras Seneda.

Akipokea pongezi hizo, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Regina  Bieda, amesema licha ya kupongezwa watahakikisha wana ongeza jitihada ili wakusanye zaidi.

Ameema katika mwaka wa fedha 2023/2024 walikisia kukusanya Bilioni 1.8, hadi kufikia mwezi Oktoba 30 walifikisha asilimia 54 hali inayowapa matumaini ya kuvuka lengo.

“Katibu tawala nashukuru kwa kutambua jitihada tunazofanya, tutaongeza juhudi zaidi, mafanikio hayo yamekuja kutokana na  ushirikiano  mzuri kati ya watumishi, madiwani na wananchi,” amesema Bieda.

Ikumbukwe kuwa katibu tawala mkoani humo, yupo kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye tarafa zote mkoani humo.alianza halmashauri ya Tunduma, Mbozi na sasa yupo Momba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

Habari Mchanganyiko

Heche ataka mawakili vijana kuamka sakata Mpoki

Spread the loveMWENYEKITI wa Mawakili Vijana Tanzania kutoka Chama cha Mawakili wa...

error: Content is protected !!