Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee, wenzake wakata rufaa kupinga hukumu ya Jaji Mkeha
Habari za SiasaTangulizi

Mdee, wenzake wakata rufaa kupinga hukumu ya Jaji Mkeha

Spread the love

HATIMAYE Mbunge wa Viti Maalumu Halima Mdee na wenzake 18 wamekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa nchini Tanzania kwa kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Jaji Cyprian Mkeha tarehe 14 Desemba 2023. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Hukumu hiyo iliwarejesha waombaji (akina Mdee) kwenye Baraza kuu la Chama cha Demokarasia na Maendeleo kusikilizwa rufaa yao ya kutofutiwa uanachama.

Rufaa hiyo imekatwa na mawakili wa Mdee na wenzie, Edson Kilatu na Ipilinga Panya tarehe 9 Januari mwaka huu katika Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam.

Itakumbukwa kuwa hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Mkeha ilibariki uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema kuwafukuza wabunge hao, huku ikibatilisha uamuzi wa Baraza Kuu la chama hicho kutupilia mbali rufaa zao walizokata kupinga kutimuliwa Chadema.

Aidha, kutokana na hukumu hiyo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilisema kitakwenda kumchongea Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, katika Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), ili avuliwe urais wake kwa madai ameshindwa kuheshimu katiba ya Tanzania,  kwa kutowaondoa bungeni wabunge viti maalum 19 waliovuliwa uanachama.

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema baada ya uamuzi huo kutoka tarehe 15 Disemba 2023, alimwandikia barua Spika Tulia akimtaka waondoe bungeni wabunge hao wakiongozwa na Halima Mdee, lakini hadi sasa hajatekeleza wito huo.

“Suala la kina Mdee tunachosubiri waondolewe bungeni, nimeshamwandikia barua spika tunataka toe kauli ya kuwoandoa bungeni. Na kama atatoa kauli tofauti ambayo itakuwa kinyume cha sheria kwa kutowaondoa tumepanga kupeleka taarifa IPU kwamba spika anavunja katiba katika nchi yake,” alisema Mnyika tarehe 20 Disemba 2024.

Hata hivyo, Wakili Kilatu alisema bado wataendelea kuwepo hadi pale baraza kuu la Chadema litakapotekeleza amri ya mahakama ya kurudia kusikiliza na kutoa uamuzi dhidi ya rufaa zao.

Wakili Kilatu alisema, kina Mdee wataendelea kubaki bungeni kwa mujibu wa kifungu cha 6C (5) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, ambacho kinasema hakuna mwanachama atakaehesabika ametukuzwa hadi michakato yote inayotambuliwa na katiba ya chama chake itakapokamilika.

“Maana yake michakato ili ikamalike inabidi mpaka rufaa ikamilike ndipo unasema mchakato wa kuwavua uanachama umekamilika. Sasa kwa sababu maamuzi ya baraza kuu tayari yamefutwa na mahakama maana yake haijaisha na chama kimeagizwa kiwasikilize upya,” alisema Wakili Kilatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

error: Content is protected !!