Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mchengerewa atangaza mabadiliko utalii, “sitaki mambo ya hovyo”
Habari za Siasa

Mchengerewa atangaza mabadiliko utalii, “sitaki mambo ya hovyo”

Spread the love

 

WAZIRI mpya wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerewa amesema kuwa kwa kushirikiana na viongozi wenzake walioteuliwa hivi karibuni atahakikisha wanafanya mabadiliko na mapinduzi makubwa katika sekta ya utalii ili ichangie zaidi uchumi wa nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo tarehe 17 Februari 2023 jijini Dodoma wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Balozi Dk. Pindi Chana.

‘’Tunahifadhi na kutangaza utalii nchini lakini pia twende tukadhibiti ujangili tunataka tudhibiti kwelikweli ili kuhakikisha kwamba vitendo vya hovyo hovyo havitokei. Na mimi kwenye kipindi changu sitotaka kusikia vitendo vya hovyo hovyo,’’ amesema Mchengerwa wakati wa makabidhiano hayo.

Aidha, Mchengerwa ameagiza kupatiwa taarifa za idara na taasisi za Wizara ifikapo tarehe 20 Februari 2023 ili aweze kuzipitia.

‘’Nataka kupitia taatifa hizi halafu tutaitana kwa ajili ya kupanga kazi tuweze kujua ndani ya kipindi cha miezi miwili tumekwendaje kwenye Wizara yetu ili tuweze kutimiza zile ndoto ambazo tunazo za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan,’’ ameongeza Mchengerwa.

Waziri huyo pia amehimiza ushirikiano baina yake na Waziri aliyekuwepo Balozi Dk. Pindi Chana.

“Naomba sana tushirikiane pale ambapo kuna jambo ambalo mnadhani nahitaji kulipitia wakati wowote . Nitaomba na wengine wakati wowote nitaomba mnipigie kama kuna taarifa ambazo ni za muhimu ili kuboresha zaidi.’’ amesisitiza Mchengerwa.

Kwa upande wake Waziri Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk. Pindi Chana amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassa kwa kuwapa dhamana ya kusimamia Wizara ya Maliasili na Utalii akieleza kuwa pamoja na kwamba sasa yupo Wizara ya Utamduni Sanaa na Michezo ataendeleza ushirikiano ili kuhakikisha Wizara zote mbili zinafanya kazi kwa pamoja.

Katika hafla hiyo pia yamefanyika makabidhiano ya ofisi baina ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Eliamani Sedoyeka na Katibu Mkuu wa sasa Dk. Hassan Abbas

2 Comments

  • KAMA BADO ANA AMINI UTI WA MGONGO NI ELIMU KWENYE LIKE JICHO TUWEKE LIKE FATHER LIKE SON (HASA KWENYE KIFO CHAO) MAANA NILILIDHI NGOMBE NA UJUZI WA KUCHUNGA NGOMBE KUTOKA KWA BABU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

error: Content is protected !!