Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Muongozo kuzuia ukatili wa kijinsi maeneo ya umma wazinduliwa rasmi
Habari Mchanganyiko

Muongozo kuzuia ukatili wa kijinsi maeneo ya umma wazinduliwa rasmi

Spread the love

 

SERIKALI imezindua mwongozo wa uanzishaji na uendeshaji wa dawati la kutokomeza ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma ili kuwasaidia wananchi kwenye maeneo hayo kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Muongozo huo umezinduliwa leo tarehe 17 Februari 2023 na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima, katika soko la Mbuyuni wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Dk. Gwajima ameitaka jamii kushirikiana kutokomeza vitendo vya ukatili kupitia kamati za ulinzi wa wanawake na watoto kwenye maeneo yao.

Amesema muongozo huo ni wa kila mdau ambaye anatekeleza ajenda ya Serikali ngazi zote yaani kuanzia wananchi wenyewe, viongozi wa Serikali ya mtaa au kijiji, watendaji wa Kata na Halmashauri na hata wanasiasa.

“Natarajia kila mdau ataona umuhimu wa kusoma na kutekeleza mpango wa ufuatiliaji ulioelezwa kwenye muongozo huu kwani utahusisha taarifa za mikoa kuwasilishwa Ofisi ya Rais TAMISEMI na kisha Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu ambapo itampelekea Waziri Mkuu ambaye, Ofisi yake ndiyo inaratibu masuala yote ya kisekta ya kupambana kutokomeza Ukatili wa Kijinsia” amesema Dk. Gwajima.

Aidha, Waziri Dk. Gwajima amehimiza Mwongozo huo kunasambazwa kila mkoa kwa kushirikiana na Wizara katika Ili kuanzisha Madawati hayo katika maeneo ya Umma.

Dk. Gwajima ameongeza kwamba, anatambua Jamii ina vipaumbele vingi ikiwemo Elimu, afya, maji, umeme, Bararara ambavyo vinavyojadiliwa kwenye vikao vya kata na vijiji na kusisitiza kuwa ajenda ya kuwalinda watoto na Wanawake iongezwe pia katika ajenda hiyo iwe ya Kudumu.

Aidha, ameishukuru Ofisi ya Rais TAMISEMI kuzielekeza mamlala za Serikali za Mitaa kuweka Sheria ndogo na kufanya ajenda ya ukatili kuwa ya Kudumu kwenye vikao vyote vya maamuzi.

“Tukaisimike ajenda hii kwenye vikao vyote, kutoijadili ni kama kuvibariki vitendo hivi kuendelea” ameongeza Waziri Gwajima.

Dk. Gwajima pia amesisitiza kuwa muongozo huo ni sehemu tu ya mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia hivyo wananchi wote washirikiane kuanzia ngazi ya familia kwa kutumia mbinu mbalimbali.

Akitoa salam za Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori amesema mkoa unaendelea kushirikiana na wadau kutokomeza vitendo vya ukatili kwa kutekeleza mipango na miongozo yote inayotolewa.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Linus Kahendaguza amesema Ofisi hiyo ina jukumu la kutekeleza Mwongozo huo kupitia watendaji wa mamlaka za Serikali za mitaa na tayari imeshaelekeza kutungwa kwa sheria ndogo za kudhibiti vitendo vya ukatili kwenye maeneo ya umma.

“Wanawake wana haki ya kujumuika kwenye mikusanyiko mbalimbali kwenye jamii lakini sehemu hizo mara nyingi Wanawake wanadhalilishwa hivyo Mwongozo huu utasaidia kupunguza au kumaliza kabisa mashambulio ya aibu” amesema Kahendaguza.

Naye Mkurugenzi wa Shirika Lisilo la Kiserikali linalojihusisha na kupinga ukatili wa kijinsia la EQUALITY FOR GROWTH(EFG), Jane Magigita amesema chimbuko la kuandaliwa kwa Mwongozo huo ni utafiti uliofanywa katika baadhi ya mikoa nchini na kubaini changamoto ya udhalilishaji wa kijinsia hasa kwa Wanawake kwenye maeneo ya Umma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!