Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa achefukwa baba aliyemlawiti mwanaye, aagiza kukamatwa, MaRC, RPC kikaangoni
Habari Mchanganyiko

Majaliwa achefukwa baba aliyemlawiti mwanaye, aagiza kukamatwa, MaRC, RPC kikaangoni

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania
Spread the love

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo wahakikishe wanamfikisha katika vyombo vya sheria baba mzazi wa mwanafunzi wa darasa la pili katika Kata ya Sokoni One mtaa wa Lonovono Jijini Arusha kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea)

Pia, amekemea vikali vitendo vya unyanyasaji, ubakaji na ulawiti kwa watoto na kuwataka Wakuu wa mikoa na makamanda wa polisi nchini wahakikishe wanawasaka na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo viovu.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo tarehe 17 Februari 2023 mkoani Songwe baada ya kusambaa kwa taarifa kupitia vyombo vya habari vikimuonesha mtoto huyo ambaye anadaiwa kulawitiwa na baba yake mzazi. Mtoto huyo ambaye alisikika akielezea namna mzazi wake huyo alivyokuwa akimfanyia vitendo vya ukatili.

Waziri Mkuu ameagiza mwanafunzi huyo pia naye atafutwe na kupatiwa huduma ya matibabu kwa haraka.

Amesema katika siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya wazazi,walezi na wanajamii kuwafanyia watoto vitendo vya ukatili ikiwemo ulawiti, hivyo kuwasababishia maumivu makali pamoja na msongo wa mawazo hali inayowafanya baadhi yao kushindwa kuendelea na masomo.

“Serikali haitosita kumchukulia hatua mzazi au mtu yeyote atakayebainika kufanya vitendo hivi vya ukatili.

“Kumeibuka wimbi la ukatili wa kuwafanyia vitendo vya hovyo watoto wetu kwenye maeneo mbalimbali nchini, hivyo fanyeni uchunguzi na kubaini wanaohusika na vitendo hivyo.

“Wakuu wa Mikoa, Makamanda wa Polisi pamoja na Maafisa wa Ustawi wa Jamii hakikisheni mnawasaka watu wote wenye tabia hizo na kuwachukulia hatua.”

Aidha, Majaliwa ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa jamii ishirikiane na Serikali katika kutokomeza vitendo vya ukatili kwa watoto na wanawake.

“Wananchi shirikianeni kuhakikisha watoto wote wanalindwa na kupatiwa haki zao za msingi, mtoto wa mwenzio ni wako.”

Amesema baadhi ya wazazi wanadhani mtoto akipelekwa shule mwenye jukumu la kumuangalia mtoto ni mwalimu pekee huku wao wakiendelea na mambo mengine ya uzalishajimali ilihali watoto wakiendelea kuharibika hasa wanaolala kwenye mabweni.

Ameongeza kuwa kumeibuka sintofahamu kwa baadhi ya taasisi hizo kufundisha watoto ambao yasiyo ya kimaadili watoto wamekuwa wakifundishwa pia kubusiana na hata mambo machafu hivyo kuna kila sababu ya wakaguzi wa shule kuvikagua vitabu na kila shule itumia vitabu vilivyoainishwa na serikali.

“Nimepita halmashauri ya Songwe,Momba na hapa nipo Tunduma, maagizo haya nimetoa katika halmashauri zote vitabu ambavyo havitakiwi viondolewe mashuleni vitolewe vitabu elekezi vya kiada na ziada,nafahamu vitabu vingi vimeingizwa mitandaoni mamlaka husika simamieni hili tuviokoe vizazi vijavyo,’’ amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!