Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: Wanaotabiri mpasuko Chadema watasubiri sana
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Wanaotabiri mpasuko Chadema watasubiri sana

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe, amesema wanaotegemea chama hicho kipasuke kutokana na migogoro watasubiri sana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 13 Januari 2024, jijini Dar es Salaam, Mbowe amesema mpasuko ndani ya Chadema haupo na kwamba kilichopo ni baadhi ya watu kutofautiana mtazamo kitu alichokiita kuwa ni afya kwa demokrasia.

“Na wale wanaofikiri kuwa chama hiki kina mgogoro watasubiri sana, wote ambao wanafikiri kuna mpasuko Chadema haupo na hautakuwepo. Tutakilinda na kukihami chama hiki kwa gharama yoyote umoja wetu ni muhimu kuliko mtu yoyote,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema “chama cha siasa ni kisima cha fikra na asitokee binadamu yoyote akafikiri kwa kuwa kwenye chama kimoja wote mtafikiri mamoja, hiyo ni kinyume na asili ya binadamu hata kwenye familia yako mnatofautiana katika masuala lakini mkiitofautiana ni afya hivyo sioni mnaonaje kuwa na viongozi na mawazo tofauti yanayokinzana eti ni mgogoro, sio mgogoro.”

Akizungumzia kuhusu Chadema kujitoa kwenye maridhiano na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbowe amesema uamuzi huo unatokana na chama chake kukosa imani dhidi yake kufuatia hatua ya Serikali iliyoko madarakani kupeleka miswada ya marekebisho ya sheria za uchaguzi ambayo haijabeba maoni yao.

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema

“Huyu mama (Rais Samia), tumekaa naye vikao  ningestahili kumuamini lakini leo nasema simuamini sababu chama chake kimepeleka miswada ambayo haiakisi zile R zake nne anazohubiri yeye na wenzake. Kiongozi unapaswa kutembea kwenye maneno yako unayotoa,” amesema Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!