Wednesday , 21 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Mbivu, mbichi sheria huduma ya habari Tanzania Juni 9
Habari Mchanganyiko

Mbivu, mbichi sheria huduma ya habari Tanzania Juni 9

Spread the love

MAHAKAMA ya Afrika ya Afrika Mashariki imeenza kusikiliza maombi ya wadau wa habari Tanzania la kutaka mahakama hiyo kufuta kusudio la Serikali ya Tanzania la kuukatia rufaa uamuzi wa mahakama hiyo wa kuondoa baadhi ya vipengele kwenye sheria ya huduma ya habari ya mwaka 2016. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Ombi hilo limesikilizwa leo Alhamisi tarehe 21 Mei 2020,  kwenye mahakama hiyo jijini Arusha.

Wadau hao ni pamoja na Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Kituo cha Sheri na Haki za Binadamu (LHRC).

Serikali ya Tanzania ilikusudia kukata rufaa kutokana na uamuzi wa mahakama hiyo wa tarehe 28 Machi 2019, wa kuviondoa  baadhi ya vifungu kwenye sheria hiyo.

Waombaji wamewakilishwa na Wakili Fulgence Massawe na Jebra Kambole. Huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na mawakili, Alicia Mbuya, Abubakari Mrisha na Stanley Kalokola.

Kutokana na Serikali ya Tanzania kutoridhishwa na uamuzi huo, ilitoa taarifa ya nia ya kukata rufaa mnamo tarehe 11 Aprili 2019.

Hata hivyo, upande wa Jamhuri haukuwahi kukata rufaa ndani ya siku 30 tangu kuonesha nia hiyo.

Kesi hii imesikilizwa kwa njia video mbele ya jopo la majaji watano wa rufaa wa Mahakama ya Afrika Mashariki na kuongozwa na Raisi wa Mahakama hiyo Jaji Emmanuel Ugirashebuja akisaidiana na  Jaji Liboire Nkurunzinza, Jaji Aaron Ringera, Jaji Geoffrey Kiryabwire na Jaji Sauda Mjasiri.

Baada ya jopo hilo kusikiliza shauri limesema litatoa uamuzi  tarehe 9 Juni 2020.

Vifungu vilivyofutwa awali ni vile ambavyo wadau hao waliviona kuwa viliwanyima wanahabari uhuru kamili wa kuwapasha wananchi habari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakazi kwa mawaziri walia majitaka kusambaa mitaani

Spread the loveWAKAZI zaidi ya 4,000 wa mitaa ya Eyasi, TPDC na...

Habari Mchanganyiko

Viumbepori, bahari hatarini kutoweka

Spread the loveKUKOSEKANA juhudi za pamoja za Serikali, wadau wa uhifadhi na...

BiasharaHabari Mchanganyiko

TPSF yataja mbinu ya kuibua vipaji vipya taaluma ya madini

Spread the loveMkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Raphael Maganga...

Habari Mchanganyiko

Kampuni 500 kushiriki maonyesho ya TIMEXPO 2024

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda nchini  ( CTI) kwa kushirikiana na...

error: Content is protected !!