Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mavunde ateta na Mwenyekiti wa bodi EITI
Habari za Siasa

Mavunde ateta na Mwenyekiti wa bodi EITI

Spread the love

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amekutana na kufanya kikao kifupi na Mwenyekiti wa Bodi ya EITI Rt. Helen Clark katika Ofisi Ndogo za Wizara  jijini Dar Es Salam. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Pia, kikao hicho kimehudhuriwa  na Katibu Mkuu  wa Wizara ya Madini Kheri Mahimbali, Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI CPA Ludovick Utouh na Katibu Mtendaji wa TEITI Bi Mariam Mgaya pamoja na viongozi kutoka Wizarani.

Akizungumza katika kikao hicho, Mavunde amesema amefurahishwa na  ujio huo na kueleza kuwa ni wa kihistoria ikiwa ni ushirikishwaji wa Sekta ya Madini katika shughuli za Uwazi na Uwajibikaji.

Aidha, kikao hicho kimekubaliana kuwa Wizara ya Madini ikishirikiana na Asasi za Kimataifa ya EITI itatimiza kikamilifu mahitaji ya matakwa ya Kimataifa ya Uwazi na Uwajibikaji katika shughuli mbalimbali za Usimamizi wa Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia nchini.

Pia Mavunde amesisitiza kwamba maoni yaliyotolewa katika ripoti ya Tathmani kuhusu Uwazi na Uwajibikaji katika nchi ya Tanzania  iliyofanyika mwaka 2023 yatafanyiwa kazi kikamilifu.

Kwa upande wake,  Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI CPA. Ludovick Utouh kwa niaba ya Katibu Mtendaji amesema dhana ya kuweka uwazi taarifa na takwimu mbalimbali za  Sekta ya Uziduaji ni kuhakikisha kuwa Rasilimali hizo zinawanufaisha wananchi na kuahidi kuwa  TEITI itatoa ushirikiano katika kutekeleza Matakwa hayo.

Ujumbe huo wa EITI ukiongozwa na Rt. Helen Clark utapata wasaa wa kukutana na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Aprili 04, 2024.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!