October 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mauaji Chicago, Trump atishia kutumia jeshi, Obama alaani

Waandamani nchini Marekani

Spread the love

MAMBO yanazidi kwenda mrama Marekani, mauaji yanaanza kushuhudiwa kwenye maandamano ya kulaani kuuawa kwa Mmarekani mweuzi, George Floyd akiwa mikononi mwa polisi. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Licha ya polisi kuwapigia magoti waandamanaji na kuwaomba msamaha, pia Tim Walz ambaye ni Gavana wa Jiji la Minnesota kueleza muuaji atachukuliwa hatua, waandamanaji wamejibu kwamba, jeshi hilo limezoea kuendesha mauaji kwa Wamarekani weusi kisha kutochukua hatua yoyote.

Makabiliano kati ya waandamanaji na polisi kwa takribani miji 75 yamekuwa makali zaidi, uharibifu wa mali na mapambano ya ana kwa ana yameshika kasi, watu wawili tayari wameuawa jijini Chicago.

Kutokana na maandamano, uharibifu na uporaji umefika kiwango cha juu kuwahi kushuhudiwa, Donald Trump, Rais wa Marekani ametishia kutumia jeshi kukabiliana na maandamano hayo.

Amesema, iwapo mameya na magavana watashindwa kutuliza ghasia hizo, atalazimika kutumua jeshi kuwakabili waandamanaji, “nitatumia jeshi haraka kurejesha amani.”

Kwenye maandamano hayo, watu wawili wanaripotiwa kuuawa katika Jiji la Chicago. Msemaji wa jiji hilo, Ray Hanania amesema, watu 60 wamekamatwa lakini hakutibitisha idadi ya watu waliofariki.

Tayari shirika la habari la Aljezeera limeripoti vifo hivyo ambapo polisi wanne wanaelezwa kushambuliwa na kuumizwa vibaya na waandamanaji katika mji huo.

Saa kadhaa zilizopita, polisi wa Washington DC wametumia maji ya kuwasha pamoja na risasi za mpira, hata hivyo, wameeleza hawaoni matumaini ya waandamanaji kurudi nyuma.

Waandamanaji hao walikuwa wanakwenda lango la Ikulu wakati Rais Trump aliokuwa kwenye mazungumzo. Polisi wameongezwa Washington kukabili wanaandamanaji kutokaribia Ikulu.

Katika miji ya Atlanta, Georgia maduka mengi yamefungwa kutokana na maandamano hayo, baadhi yao waandamanaji wamevunja vioo na kuingia ndani kisha kupora.

Mamlaka za miji hiyo zimeendelea kulinda maeneo ya huduma za umma ili zisiharibiwe, waandamanaji wanaendelea na maandamano bila kujali tishio kubwa la virusi vya corona.

Matumizi ya risasi za moto na maji ya kuwasha yamekuwa kwa kiwango kikubwa, watu kadhaa wanashikiliwa na polisi.

Mpaka kufikia usiku wa kuamkia leo Jumanne tarehe 2 Juni 2020, watu 5,600 wanaripotiwa kuwekwa nguvuni na polisi kutokana na maandamano hayo.

Minnesota ambapo Floyd alifariki dunia, watu 155 tayari wamekamatwa, New York 800 na zaidi ya watu 900 wamekamatwa Los Angeles.

Siku moja baada ya waandamanaji kushambulia kanisa la kihistoria la St John’s Episcopal lililopo Washington DC karibu na Ikulu, Trump amekwenda kutembelea na kuangalia uharibifu uliofanywa.

Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama amepongeza maandamano yanayolenga kumaliza ubaguzi wa rangi nchini humo.

Hata hivyo, amekosoa vikali vurugu zinazofanywa na waandamanaji.

Obama amewataka waandamanaji kuhakikisha wanachagua viongozi ambao wanaweza kuhakikisha maujai ya namna hiyo yanakomeshwa.

error: Content is protected !!