Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Gazeti la MSETO lashinda kesi tena mahakamani
Habari Mchanganyiko

Gazeti la MSETO lashinda kesi tena mahakamani

Spread the love

MAHAKAMA ya Rufaa ya Afrika Mashariki (EAC), imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Jamhuri dhidi ya gazeti la kila wiki la MSETO, kupinga gazeti hilo kuendelea kuchapishwa. Anaripoti Mwandidishi Wetu, Arusha … (endelea).

Taarifa kutoka jijini Arusha, nchini Tanzania, ambako mahakama hiyo inafanyia shughuli zake zinasema, uamuzi wa kutupilia mbali maombi hayo, umefanyika leo Jumanne, tarehe 2 Juni 2020.

Wakili wa gazeti la MSETO ambalo linachapishwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited (HHPL), Fulgence Masawe, ameiambia MwanaHALISI ONLINE, kwamba serikali imezembea katika shauri inayolihusu yenyewe.

Amesema, “ni kweli kwamba leo Jumanne (tarehe 2 Juni 2020), Mahakama ya Afrika Mashariki, imefuta Notice of Appeal (kusudio la kukuta rufaa) la Serikali ya Tanzania katika shauri Na. 3 la mwaka 2019.”

Kwa mujibu wa Masawe, Mahakama imetupilia mbali pia maombi ya Serikali kuongezewa muda wa kukata rufaa nje ya muda kama ambavyo serikali iliwasilisha mahakamani.

Katika shauri hilo lililoendeshwa kwa njia ya mtandao – Video Conferencing – gazeti la MSETO liliwasilisha maombi mahakamani, “kufutilia mbali, kusudio la serikali ya Tanzania, kukata rufaa.”

Serikali iliwasilisha maombi hayo, kupinga maamuzi ya Mahakama Kuu ya Afrika Mashariki, kwenye shauri Na 3 ya mwaka 2019, yaliyoipa ushindi gazeti la MSETO na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya HHHP Limited.

 

Gazeti la MSETO lilipigwa marufuku ya kuchapisha yoyote ile na kuisambaza kwa muda wa miaka mitatu tangu 11 Agosti 2016.

Serikali ilieleza wakati huo, kwamba imelazimika kuchukua hatua hiyo, kufuatia gazeti “kuchapisha habari za uongo na kuchochea machafuko.”

Habari iliyosababisha MSETO kufungiwa ni ile iliyodai kuwa mmoja wa watendaji wa serikali wa wakati huo, alikubali kupokea hongo ili kufadhili kampeni za urais, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Katika uamuzi wake wa awali, Mahakama Kuu ya Afrika Mashariki, ilibaini kwamba serikali ya Tanzania, “haikuonyesha jinsi makala hayo yaliyochapishwa gazetini, yalikiukwa maslahi ya umma au kuhatarisha amani na usalama wa raia.”

Majaji walihitimisha kuwa uamuzi wa kufungwa kwa gazeti hilo uliochukuliwa na wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania, ulichukuliwa “kwa ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa kujieleza,” na kuamuru gazeti la Mseto “kuendelea na kazi yake.”

Akizungumzia maombi mengine ya serikali ambayo yalisikilizwa sambamba na maombi ya MSETO ya kufutwa kwa maombi ya serikali, Masawe amesema, mahakama hiyo pia imekatalia serikali, kuwasilisha rufaa nje ya muda.

“Majaji wamesikiliza pia hoja za serikali katika shauri Na. 4 la mwaka 2019, yaliyowasilishwa na wadaiwa wakiomba kupewa muda wa kuleta rufaa nje ya muda wa kisheria,” ameeleza Masawe.

Amesema, “Mahakama imesema, haikuona kokote ambako kulikuwa na sababu za msingi kwa serikali kutowasilisha kesi yake ndani ya muda uliowekwa.”

Maombi hayo yalifunguliwa na gazeti la MSETO, mhariri mtendaji wa gazeti hilo na kampuni ya HHP Limited, ilisikilizwa na jopo la majaji watano (5) wa Mahakama ya Rufaa, wakiongozwa na Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Emmanuel Ugirashebuja.

Majaji wengine waliokuwamo kwenye kesi hiyo, ni pamoja na Makamu wa Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Liboire Nkurunzinza; Jaji Aaron Ringera, Jaji Geoffrey Kiryabwire na Jaji Sauda Mjasir.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!