Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mashtaka ya Mbowe yawaibua CUF, wamwangukia Rais Samia
Habari za Siasa

Mashtaka ya Mbowe yawaibua CUF, wamwangukia Rais Samia

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, aingilie kati sakata la kushikiliwa kwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, anayekabiliwa na tuhuma za ugaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumatano, tarehe 28 Julai 2021 na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Mhandisi Mohamed Ngulangwa, akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

“Pamoja na kutotaka kuingilia masuala ya kiupelelezi yanayofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama,”

“Kukamatwa kwa Mbowe na hatimae kuhusishwa na ugaidi, kunaweza kutafsirika ni muendelezo wa matukio ya kubambikiza kesi, jambo ambalo Rais Samia amelikataza kwenye hotuba zake,” amesema Ngulangwa.

Ngulangwa amesema mashtaka aliyofunguliwa Mbowe yana mashaka, kutokana na kuwa tofauti na sababu za kukamatwa mwanasiasa huyo Mwanza.

“Jeshi la Polisi lilijitokeza hadharani na kueleza kwamba, sababu za kumshikilia Mbowe ni tuhuma za ugaidi zinazomkabili muda mrefu ambazo zinahusisha kuua au kutaka kuua viongozi kadhaa wa Serikali,” amedai Ngulangwa.

Msemaji huyo wa CUF amesema “hata hivyo, kwa mujibu wa hati ya mashtaka kwenye kesi ya uhujumu uchumi No. 63/2020 hakuna hilo la mauaji ya viongozi wa Serikali.”

Mbowe alikamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, usiku wa kuamkia tarehe 21 Julai 2021, akiwa katika Hoteli ya Kingdom jijini humo, akijiandaa kushiriki kongamano la katiba mpya, lililoandaliwa na Chadema.

Baada ya kukamatwa Mwanza, Mbowe alipelekwa katika Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaaam na kuhojiwa kwa tuhuma za ugaidi.

Mbowe alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, jana tarehe 26 Julai 2021 na kusomewa mashtaka ya uhujumu uchumi na ugaidi.

Kwa mujibu wa mashtaka hayo, Mbowe anadaiwa kula njama na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi.

Rais Samia Suluhu Hassan

Mwanasiasa huyo alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba, na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ester Martin, akisaidiwa na Tulimanywa Majigo.

Inadaiwa kuwa, Mbowe alitenda makosa hayo kati ya Mei na Agosti 2020, kwenye Hoteli ya Aishi, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kesi ya Mbowe, inatarajiwa kusikilizwa tena tarehe 5 Agosti 2021, baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha nyaraka muhimu katika Mahakama Kuu, kwa ajili kusomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo.

Mbowe alifikishwa mahakamani siku tano, tangu alipokamatwa akiwa katika Hoteli ya Kingdom jijini Mwanza, usiku wa kuamkia tarehe 21 Julai mwaka huu, akijiandaa kushiriki kongamano la kudai katiba mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!