SERIKALI ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluh Hassan imetoa zaidi ya Sh bilioni 4.7 katika kuboresha huduma za afya halmashauri ya wilaya ya Kigoma na kuwezesha wananchi kuanza kupata huduma maeneo ya karibu. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).
Akizungumza leo tarehe 15 Desemba 2023, ofisini kwake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Rose Manumba amemshukuru Rais Samia kwa kuonyesha upendo kwa wananchi wa Kigoma ambapo kwa miaka mitatu sekta hiyo ya afya imebadilika kwa ukubwa wake.
Aidha, amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kimewezesha halmashauri hiyo kujenga vituo vitatu vya afya vipya, Hospitali ya wilaya sambamba na zahanati ambapo wananchi kwa sasa hawatembei umbali mrefu kuzifuata huduma hizo tofauti na ilivyokuwa miaka mitatu nyuma.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi katika halmashauri hiyo wameipongeza serikali kwa kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu wa kufuata huduma za afya ambapo wameelezea kuwa kwa kipindi cha nyuma wanawake wengi walikuwa wakijifungulia njiani wakipelekwa kwenye zahanati za mbali na maeneo yao
James Kayunguye ni mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma ambaye amesema kuwa sekta ya afya katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma imeimarika Zaidi kwa kuongezeka kwa vituo vya afya na zahanati hasa katika mwambao wa ziwa Tanganyika.
Leave a comment