Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Malkia Elizabeth, mwanaye, mkwewe wapata Corona
Habari MchanganyikoKimataifa

Malkia Elizabeth, mwanaye, mkwewe wapata Corona

Spread the love

LICHA ya kupata chanjo tatu za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona, janga hilo limebisha hodi katika familia ya Malkia Elizabeth wa Uingereza baada ya yeye, mwanaye wa kwanza na mkwewe kupata maambukizi ya virusi hivyo kwa nyakati tofauti. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Jana tarehe 20 Februari, 2022 kasri la Buckingham ambalo ni makazi ya makia huyo limesema, kiongozi huyo ana dalili za kawaida kama za mafua.

Malkia ambaye tarehe 21 Aprili mwaka huu anatarajiwa kufikisha miaka 96, alikuwa akiwasiliana na mtoto wake mkubwa ambaye ndiye mrithi wake, Prince wa Wales.

Prince Charles (73) alikutwa na maambukizi ya virusi vya Corona wiki iliyopita ilihali mkewe Camila mwenye umri wa miaka (74) naye akikutwa na virusi hivyo.

Hadi sasa inaelezwa kuwa watu kadhaa wamepima virusi katika makazi ya Malkia.

Kasri la Buckingham limesema kwamba kiongozi huyo ataendelea kufanya shughuli zake nyepesi katika Kasri la Windsor katika kipindi cha wiki chache zijazo na ataendelea kutibiwa na kufuata miongozo yote ya kupambana na maambukizi vya virusi vya Corona.

Malkia Elizabeth tayari amepata chanjo tatu dhidi ya COVID. Malkia alipokea chanjo yake ya kwanza ya Covid tarehe 9 Januari 2021.

Hao yanajiri wakati serikal ya Uingereza inayongozwa na Waziri Mkuu, Boris Johnson ikijipanga kuondoa vikwazo vyote vya Covid -19.

Wiki hii Serikali hiyo inatarajia kuondoa vizuizi vyote vilivyosalia vya kupambana na maambukizi katika mkakati wake wa kuishi na virusi vya Corona.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!