Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Shaka amfagilia Rais Samia kuitangaza Tanzania
Habari za SiasaTangulizi

Shaka amfagilia Rais Samia kuitangaza Tanzania

Spread the love

 

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi, Shaka Hamdu Shaka amesema chama hicho kinaridhishwa na juhudi za kisera zitokanazo na upeo, uthubutu na juhudi zinazochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika medani za kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Aidha, kimesema kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia sio ndogo kwani amefanikiwa kuithibitishia dunia msimamo wa taifa, sera za serikali yake kama fahari ya Tanzania na Afrika.

Msimamo huo umetolewa leo Jumapili, tarehe 20 Februari 2022, katika uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere jijini Dar Es Salam mara baada ya Rais Samia kuwasili nchini alipomaliza kutembekea mataifa ya Ufaransa na Ubelgiji.

Shaka amesema Rais Samia licha ya kuonesha kwake upeo, maarifa na ufahamu mpana, aliweka bayana msimamo wa nchi yake wenye dhamira ya kudunisha kuendeleza ushirikiano wa kikanda na kimataifakwa

“Rais Samia kila alipopita akikutana na wakuu wa nchi wenzake, pia alikutana na makundi mbali mbali na kutoa hotuba za kizalendo akiweka msisitizo wa masheikiano ya kikanda na kimataifa na kumfanya ajipambanue kimataifa,” amesema

“Rais samia ni alama mpya ya nchi yetu na kioo cha Afrika kwenye medani za kimataifa. Amekuwa mchapakazi anayesimamia utekelezaji wa sera zilizomo kwenye ilani ya Uchaguzi,” amesema Shaka.

Amesema Chama Cha Mapinduzi toka awali hakikukosea kumfanya Makamo wa Rais na sasa ni Rais. CCM hakina hofu naye hata aliposhika urais baada ya kifo cha Hayati Dkt John Magufuli .

Amesema kwa jinsi anavyoendelea kuchapakazi amethibitisha ni kiongozi mwenye uwezo na uelewa huku akimudu vyema kutekeleza majukumu yake na kuonyesha dhamira alionayo.

“Watanzania wamejawa furaha na matumaini kadri wanavyomuona kingozi wao akihangainja huko na huko.Amefanikiwa kukubalika kimataifa pia akikiniwa na jumuiya za kimataifa, taasisi za fedha na mashirika ya kimaendeleo,” amesema shaka.

 

Aidha amesema sera ya Mambo ya nje ya Tanzania imelenga kuendeleza diplomasia ya uchumi baada ya kupata mfanikio makubwa ya kujitangaza mimataifa, kuelezea sera na misimamo yake tokea awamu ya kwanza hadi ya sita.

Shaka amesema, Rais Samia amejenga ukuribu na viongozi wa mataifa yenye uchumi imara duniani baada na kufanikiwa kukutana na marais wenzake kadhaa kutokana na msingi uliowekwa watangulizi wake.

“Rais Samia itakumbukwa slianza kuzuru nchi za jumuiya ya afrika Mashariki kabla hajatembea mataifa ya ulaya na marekani.Amelihutubia baraza la usalama la umoja wa mataifa pia kukutana na jumuiya za kimataifa,” amesema

“Kama nilivyosema Rais hatazuiwa kwenda mahali popote.Hatafanya hivyo kwasabu dunia ya sasa si ile ya Rais kujifungia ikulu.Anapaswa kuingia kwenye mawindo ya diplomasia ya uchumi. Ulimwengu wa leo ni kijiji kimoja kinachotegemeana na wala si muda wa kujitenga,” amesema Shaka

Shaka amesema Rais samia amekuwa akishiriki kwenye meza na majukaa mvalimbali ya majadiliano ya kisiasa ,kibiashara na ya kiuchumi kwa manufaa ya watu wake taifa lake.

Amesema kutokana na juhudi hizo ameweza kufanikisha na kupata misaada ya fesha za maendeleo ya kisekta ambayo itasukuma mbele sekta za umma kilimo, afya,elimu mazingira ,mapambano dhidi ya uviko 19 mabadiliko ya tabia nchi.

2 Comments

  • Hiyo ni misaada au mikopo? Kwanini hamtaki kusema ukweli? Acha wananchi wajue ukweli pamoja na masharti ya mikopo/ MSITUFICHE BALI TANGAZA HIYO MIKATABA MLIYOSAINI HUKO ULAYA
    Je tuna mkakati wa kuzilipa? Au ni kuongeza tozo?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!