September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Balozi Kagasheki ampa heko Rais Samia, amtaja Magufuli

Spread the love

KADA mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kurejesha uhusiano mwema kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) baada ya kutetereka katika Serikali ya Awamu ya Tano. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Balozi Kagasheki ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter leo tarehe 21 Februari, 2022 na kueleza kuwa amefurahi kuona Rais Samia ameachana na baadhi ya misimamo ya hayati Rais John Magufuli.

“Inafurahisha kuona Rais Suluhu Samia akiachana na misimamo ya Magufuli ya kujitenga kwa kuirejesha Tanzania katika masuala ya kimataifa ambayo ni msingi wa sera yetu ya mambo ya nje tangu tupate uhuru,” ameandika Balozi Kagasheki ambaye alikuwa Mbunge wa Bukoba Mjini (CCM) kuanzia 2005 -2015 kabla ya kuangushwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kulipoteza jimbo hilo kwa Wilfred Lwakatare (Chadema).

Kauli hiyo ya Balozi Kagasheki ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, imekuja siku moja baada ya Rais Samia kuelezea mambo aliyoyafanya katika ziara yake huko Barani Ulaya katika nchi za Ubelgiji na Ufaransa.

Jana tarehe 20 Rais Samia alisema katika ziara na mikutano aliyoifanya Barani Ulaya imeifanikisha Tanzania kukwamua miradi iliyokuwa imekwama.

Akizungumza na wananchi waliokwenda kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Rais Samia alisema miradi hiyo ilikwama katikati baada ya kuwachokozana kidogo Umoja wa Ulaya na kusababisha uhusiano kati ya Tanzania na umoja hu kutetereka.

“Lakini pia tumeweza kuikwamua miradi iliyokuwa imekwama, kama mnavyojua katikati hapa tulichokozana kidogo na Umoja wa Ulaya uhusiano ukatetereka miradi ikakwama.

“Tulikuwa na mradi wa kujenga Airport za nadhani za Kigoma, Shinyanga na Pemba, lakini pia mradi wa Green Cities ambao Pemba, Kigoma na mji mwingine pesa zao zilikwama lakinbi tumeshakwamua. Mradi mmoja umeshatiliwa na mwingine itatiwa hivi punde kazi zitaendelea,” alisema Rais Samia.

error: Content is protected !!