Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Makatibu wakuu SADC wakutana kujadili usalama DRC
Habari za Siasa

Makatibu wakuu SADC wakutana kujadili usalama DRC

Spread the love

KATIBU Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Samwel Shelukindo ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kamati ya Utatu ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa mtandao. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).


Balozi Shelukindo ameshiriki katika Mkutano huo akiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano umejadili hali ya ulinzi na usalama mashariki mwa DRC.

Mkutano huo umefuatiwa na Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC (SADC MCO) ambapo ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Stergomena Tax kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!