WAZIRI wa Nishati January Makamba ameeleza kuridhishwa na kasi ya ujazaji maji Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere Hydro Power.
Kwa sasa ujazo wa maji umefika mita za ujazo (Cubic Meters) Bilioni 6. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Amesema zimebaki mita 13 kufikia kiwango cha maji yatakayoweza kuzungusha mitambo ya kufua Umeme.
Makamba ametoa kauli hiyo leo tarehe 25 Aprili 2023 alipofika kwenye mradi wa bwawa hilo lililopo Rufiji mkoa wa Pwani kukagua hatua na maendeleo mbalimbali yanayoendelea kufanyika kwenye mradi huo.
Amesema kuwa kiwango hicho ni kizuri na kimezidi matarajio yaliyokuwepo awali wakati wa uzinduzi wa ujazaji maji uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.
“Maendeleo ni mazuri ingawa kazi bado ipo. Kwa mujibu wa takwimu, kiwango cha maji yaliongia wiki mbili zilizopita, ni mengi kuliko maji yaliyoleta mafuriko 2019/2020. Hii maana yake ni kwamba kwa neema ya mvua iliyopo kwa sasa, zile athari za mafuriko zilizokuwepo siku za nyuma hazipo tena.
“Bwawa hili limeanza kuzaa matunda tuliyotarajia ikiwemo kudhibiti mafuriko. Kwa sasa ujenzi wa bwawa kwa ujumla uko asimilia 85.06. Wakati Rais Samia anachukua madaraka ya nchi mradi huu ulikua ni asilimia 37″ – Waziri Makamba.
Leave a comment