Saturday , 2 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Majeshi Israel yatua nyumbani kwa kiongozi wa Hamas
KimataifaTangulizi

Majeshi Israel yatua nyumbani kwa kiongozi wa Hamas

Spread the love

Jeshi la Israel limesema limeyashambulia makazi ya kiongozi wa kisiasa wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh katika Ukanda wa Gaza. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Jeshi hilo limedokeza kuwa makazi hayo yalikuwa yakitumika kama sehemu ya miundombinu ya kigaidi.

Jeshi hilo limesema makazi hayo yalikuwa yakitumika kama sehemu ya miundombinu ya kigaidi na mara kwa mara yalitumika kama eneo la mikutano ya viongozi wa juu wa Hamas.

Jeshi la Israel limebainisha kwamba ndege zake za kivita zimeyashambulia maaazi ya Ismail Haniye anayeongoza Ofisi ya masuala ya kisiasa ya kundi la Hamas.

Taarifa za mashambulizi hayo zimetolewa katika chapisho lililoambatana na video ya mashambulizi hayo katika ukurasa wa jeshi la Israel la mtandao wa kijamii wa X uliokuwa ukijulikana awali kama twitter. 

Hata hivyo, duru za habari zinasema, Haniyeh, ambaye makazi yake yamelengwa na mashambulizi ya Israel amekuwa akiishi nchini Qatar tangu mwaka 2019 pamoja na familia yake.

Kulingana na ripoti kutoka vyanzo ndani ya Hamas, hakukuwa na mtu ndani ya nyumba hiyo wakati wa mashambulizi.

Wakati hayo yakijiri, Rais wa Israel, Isaac Herzog amezungumzia mustakabali wa hali ya usalama ya Ukanda wa Gaza inavyoweza kuwa hapo baadaye.

Herzog amesema Israel haiwezi kuondoka kirahisi Gaza kwani eneo hilo haliwezi kuachwa namna lilivyo sasa.

Amefafanaua zaidi na kuongeza kuwa ili kuzuia ugaidi kujitokeza tena, wanapaswa kuwa na kikosi madhubuti kuhakikisha kuwa shambulio kama la Oktoba 7 halijitokezi tena.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Kimataifa

Israel yarejesha mashambulizi Gaza ikilaumu Hamas kukiuka makubaliano

Spread the loveJESHI la Israel, limerejesha mashambulizi katika ukanda wa Gaza, baada...

Kimataifa

Papa Francis kumfukuza Kardinali anayepinga mageuzi Kanisa Katoliki

Spread the loveKIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, anadaiwa kupanga kumfumkuza...

Habari za SiasaTangulizi

⁩ Samia aridhia Chongolo kujiuluzu

Spread the loveMwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano ameridhia...

error: Content is protected !!