Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameeleza kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu wakiwemo mawakala feki wa mbole ‘vishoka’ wanaotorosha mbolea ya ruzuku kwenda nchini Malawi na kusisitiza kuwa watuhumiwa hao ni sawa na wauaji. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).
Majaliwa ameyasema hayo leo tarehe 24 Novemba 2023 katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Ileje mkoani Songwe alipokuwa akizungumza na wananchi.
Amesema Serikali inawajali wakulima ndiyo maana imeletea mbole ya ruzuku ambayo kila mfuko mmoja wa mbolea una thamani ya Sh 50,000 ya Serikali.
“Mwaka jana walikamatwa watu kadhaa wakitorosha mbolea kwenda Malawi, adhabu kubwa itatolewa dhidi yao nawasihi wananchi acheni vitendo hivyo mtafungwa,” amesema Majaliwa.
Naye Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga (CCM) amewapongeza wana-Ileje kwa kulima mazao mengi ya chakula na biashara lakini anashangaa kuona hawajui kutumia mazao hayo.
Amesema kitendo cha wananchi kulima mazao mengi alafu wanakuwa na kiwango kikubwa cha utapiamlo kinaitia aibu Ileje.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema kwa kushirikiana na uongozi wa halmashauri pamoja na mkuu wa wilayani watahakikisha wana wasimamia wananchi ili wapate mbolea.
Amesema kumekuwa na malalmiko kila kona kuhusu wakulima kutofikiwa na mbolea za ruzuku huku wakiendelea kuuzia mbolea kwa bei juu na mawakala vishoka.
Leave a comment