Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Mahakama Uganda yafuta sheria ya tata ya mawasiliano
Kimataifa

Mahakama Uganda yafuta sheria ya tata ya mawasiliano

Spread the love

 

MAHAKAMA ya Katiba nchini Uganda jana tarehe 10 Januari, 2023 imefuta sehemu ya sheria ya mawasiliano ambayo imekuwa ikitumika kuwashtaki wakosoaji wa serikali, waandishi habari na waandishi wa vitabu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Sehemu ya sheria hiyo ya matumizi mabaya ya Kompyuta, ilikuwa inakataza matumizi ya mawasiliano ya kieletroniki kuvuruga amani, utulivu au haki ya faragha ya mtu yeyote asiye na kusudio la kufanya mawasiliano.

Adhabu ya wanaokiuka sheria hiyo ilikuwa ni faini ya fedha na kifungo cha hadi miaka saba gerezani.

Katika uamuzi wa kesi hiyo iliyofunguliwa na mwanaharakati mmoja nchini Uganda, Mahakama ya Katiba imekubali ombi hilo na kusema sehemu hiyo ya sheria inakiuka katiba.

Jaji wa Mahakama ya Katiba, Kenneth Kakuru amesema kifungu hicho cha sheria ni batili, kwani kinabinya uhuru wa kujieleza katika jamii huru na ya kidemokrasia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Ramaphosa akiri tatizo la umeme Afrika Kusini kuathiri sekta ya madini

Spread the love  RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema tatizo la...

Kimataifa

Idadi ya vifo tetemeko la ardhi yafikia 9000

Spread the love  IDADI ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi Uturuki: Vifo vyaongezeka hadi 4,800

Spread the love  Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko lililotokea jana Jumatatu...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi laua watu 300 Uturuki, Syria

Spread the love  WATU  300 wamefariki dunia katika tetemeko kubwa la ardhi...

error: Content is protected !!