Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Machinga mbaroni kwa wizi wa kichanga cha siku 21
Habari Mchanganyiko

Machinga mbaroni kwa wizi wa kichanga cha siku 21

Spread the love

JESHI la POLISI Mkoa wa Songwe linamshikilia Praxeda Msanganzila (28) Mkazi wa mtaa wa Ilolo, wilayani Mbozi kwa tuhuma za kuiba mtoto mdogo Mudrick Shula (siku 21). Anaripoti Moses Ng’wat, Songwe… (endelea).

Mtuhumiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara wa kuuza nguo mtaani (machinga) alifanikisha wizi huo baada ya kumlaghai mama mzazi wa mtoto huyo  Antifonia Mdolo (21) Mkazi wa mji mdogo wa Mlowo, Wilayani Mbozi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe, Alex Mkama,  alisema wizi huo ulitokea tarehe 12 Disemba mwaka huu, muda wa saa 12:00 jioni katika mtaa wa Tazara katika Mji mdogo wa Mlowo, Wilayani Mbozi.

Akieleza mazingira ya wizi huo, Kamanda Mkama alisema mtuhumiwa alimdanganya mama wa mtoto huyo baada ya kumuomba amsaidie kutafuta nyumba ya kupanga.

Alisema baada ya mtuhumiwa kufika nyumbani kwa mama mazazi wa kichanga huyo aliyeibwa alitengeneza urafiki wa muda mfupi hali iliyofanya mama wa mtoto huyo amuamini.

“Mtuhumiwa alifika nyumbani  kwa mama wa mtoto (kichanga)  na kuulizia vyumba vya kupanga na wakiwa wanaelekea kutafuta vyumba hivyo aliomba ambebe mtoto na baadae alitoweka katika mazingira ya kutatanisha” alifafanua Kamanda Mkama.

Alisema baada ya mtuhumiwa kutoweka na mtoto huyo mama wa mtoto alitoa taarifa polisi na kuanza msako wa kumtafuta mtoto huyo ambaye alipatika siku inayiofuata.

“Tumefanikiwa kumkata mtuhumiwa akiwa na mtoto huyo ndani ya nyumba yake baada ya majirani kutoa taarifa polisi kufuatia kelele za kulia kwa mtoto usiku kucha,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

error: Content is protected !!