Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mabadiliko ya tabiachi yaathiri Tanzania
Habari Mchanganyiko

Mabadiliko ya tabiachi yaathiri Tanzania

Hali ya ukame katika moja ya maeneo ya Afrika kwa sasa
Spread the love

UTAFITI uliyofanywa na Mtandao wa Jinsia na Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania (GCCTC), umebaini kuwa kila eneo katika nchi ya Tanzania limeathirika na mabadiliko ya tabianchi kwa namna tofauti. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Ili kukabiliana na janga hilo na kusaidia mapambano yanayoendelea sasa, utafiti huo umeishauri Serikali kufanya mchakato kwa lengo la kupatikana kwa sheria na kanuni zinazozungumza lugha moja.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo tarehe 13 Disemba, 2022 katika uzinduzi wa utafiti huo uliyopewa jina la Mabadiliko ya Tabianchi Jinsia na Haki za Binadamu, Mratibu wa Mtandao huo, Maria Matui alisema Tanzania ni kubwa na kila eneo la nchi limeathirika na mabadiliko ya tabianchi nchi kwa namna tofauti.

Alisema jamii inayozunguka maeneo hayo wakiwemo vijana, wazee,  walemavu, wanawake na watoto wamekuwa wakiathirika na mabadiliko hayo hivyo ni muhimu kuwepo kwa sheria na kanuni zinazoendana ili kuweza kukabiliana na janga hilo.

“Hata hivyo changamoto ambayo tumeiona bado uelewa kwa jamii kuhusu mabadiliko haya ya tabianchi ni mdogo licha ya jitihada zilizopo Serikalini na asasi za kiraia, makundi haya ya vijana, wazee, watoto na wanawake yanaathirika na hata jinsi ya kuyahimiri imekuwa ni shida,” alisema Matui.

Aidha, alisema utafiti huo ulianza kuandaliwa Julai, mwaka huu huku wakiwa na lengo la kuangalia chagamoto pamoja na fursa zilizopo katika nyaraka mbalimbali za serikali ambazo zimeweka miongozo ya mabadiliko ya tabianchi na jinsia.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Vijana na mwanachama wa mtandao huo, Humphrey Mrema alisema wameshirikishwa katika mchakato mzima wa kuandaa utafiti huo ambao unalenga pia kujua mapungufu yaliyopo katika sera zilizopo kwa ajili ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

“Kwa takwimu zilizotolewa na serikali zaidi ya asilimia 60 ya watanzania ni chini ya umri wa miaka 35, maana yake hatuwezi kufanya matumizi ya kitaifa bila kuwashirikisha vijana, sasa hivi watu wanasumbuliwa na ukosefu wa maji,  umeme na ukame.

“Majanga haya yanapotokea wanaoathirika zaidi ni wanawake,  watoto, wazee na vijana, tunazo sera ambazo zingine zipo katika mpango wa nchi na Afrika nzima,  ila katika sera hizo yapo mambo ambayo tumeona yanahitajika kubalishwa ili kurahisisha ushiriki wa vijana uongezeka,” alisema

Kwa upande wake Neema Olendino kutoka Shirika la Kutafuta Taarifa na kufanya Utafiti juu ya masuala ya wafugaji Tanzania, alisema mabadiliko ya tabianchi ni moja ya changamoto kubwa inayoikabili nchi na dunia kwa ujumla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!