Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mabadiliko sheria ya uchaguzi, vyama vya siasa kutua bungeni mwaka huu
Habari za Siasa

Mabadiliko sheria ya uchaguzi, vyama vya siasa kutua bungeni mwaka huu

Jenista Mhagama
Spread the love

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Jenister Mhagama amesema kabla ya mwaka huu 2023 kumalizika, Serikali itakuwa imepeleka bungeni Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Msajili wa Vyama vya Siasa ili zifanyiwe kazi na kupitishwa na Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hatua hiyo imekuja ikiwa zimepita siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kuitishia mkutano wa wadau kupitia Baraza la Vyama vya siasa kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya kikosikazi kilichoratibu maoni kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini pamoja na kuanza mchakato wa Katiba mpya.

Akichangia mjadala kuhusu hotuba ya bajeti ya wizara ya kilimo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 leo tarehe 8 Mei 2023 bungeni jijini Dodoma, Mbunge wa Kiteto, Edward Kisau (CCM

Mbunge wa Kiteto, Edward Kisau (CCM)

) mbali na kumpongeza Rais Samia kwa hatua hiyo, pia aliitaka serikali iharakishe kupeleka mabadiliko hayo ya sheria bungeni.

“Nimpongeze kwa suala la Katiba mpya, naomba serikali sasa ilete mabadiliko ya sheria hizi ili kuweka miundombioni vizuri kwa ajili ya kujiandaa na zoezi hilo-  Sheria ya tume ya uchaguzi na vyama vya siasa,” amesema.

Wakati akiendelea na mchango wake, Mhagama aliomba kutoa taarifa kwa mbunge huyo ambapo pamoja na mambo mengine alisema Serikali tayari imekwishajipanga kwa ajili ya kukutana na wadau.

“Naomba nimhakikishie kwa tamko la rais la tarehe 6 Mei mpaka sasa, ofisi ya rais, waziri mkuu, msajili, tume ya uchaguzi, tayari imeshajipanga kuitisha kikao cha wadau kupitia baraza la vyama vya siasa  kuhakikisha mchakato wa Katiba mpya unaendelea.

“Kuhusu sheria hizi nimhakikshie kwamba kabla ya mwaka huu wa 2023  kuisha, sheria hizi pia zitakuwa zimekwisha kufanyiwa kazi kusudi kila jambo liweze kwenda kwa wakati,” amesema Mhagama.

Aidha, Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu amesema Rais Samia anastahili kupongezwa kwa hatua hiyo lakini Mbunge huyo wa Kiteto akaongeza kuwa namna bora ya kumpongeza mkuu huyo wa nchi ni kuleta sheria hizo kwa haraka kwani wazisubiri kwa hamu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!