Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lowassa atema nyongo Z’bar
Habari za Siasa

Lowassa atema nyongo Z’bar

Umati wa watu uliofika katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar
Spread the love

EDWARD Lowassa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, amesema bao la mkono la Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ndilo lililompa ushindi Rais John Magufuli, anaandika Mwandishi Wetu.

Lowassa kwenye uchaguzi huo aligombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Ametoa kauli hiyo jana alipokuwa kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar.

Mgombea huyo aliyeungwa mkono na vyama Ukawa amesema kwamba, anaamini alimshinda Dk. John Magufuli ila ushindi wake uliporwa.

Kwenye mkutano huo Lowassa ameongeza kuwa, licha ya kujua ameporwa ushindi wake alikaa kimya kwa lengo la kuepusha vurugu.

Jana CUF kilifanya uzinduzi wa kampeni kwenye jimbo hilo ukiongozwa na Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF pamoja na Lowassa. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Fuoni.

Akimnadi mgombea ubunge wa CUF, Abdulrazaq Khatibu Ramadhani Lowassa amesema “niwahakikishie Watanzania kwamba Ukawa tulishinda.”

Amesema kuwa, mgombea wa CCM alishindwa kwa bao la mkono na kwamba, pamoja na kuzongwa na makundi ya vijana kutokana na kuporwa ushindi wake, aliamua kuiepusha nchi na matatizo.

Kiongozi huyo amesema kuwa, hatua ya Rais Magufuli kuendesha nchi kwa vitisho na ubabe kunatokana na kutojiamini kwa kuwa, alishinda kwa bao la mkono.

Pamoja na hivyo amesema kuwa, Serikali ya Rais Magufuli licha ya kuendesha mapamano mbalimbali lakini inaelekea kukwama huku akitolea mfano hali mbaya ya uchumi kwa wananchi.

Amewahakikishia Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kuwa, mabadiliki makubwa yanakuja na kwamba, mwaka 2020 CCM itang’oka.

Hata hivyo amewataka CUF kutokubali tena kuibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Kauli hiyo inakuja huku CUF ikiwa na malalamiko ya kuibiwa kura kila baada ya uchaguzi mkuu kufanyika visiwani humo.

Wapenzi, wanachama na viongozi wa chama hicho visiwani Zanzibar wanaamini kwamba, tangu uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi visiwani humo mwaka 1995, chama hicho kimekuwa kikishinda lakini kimekuwa kikiporwa na chama tawala (CCM).

Kulingana na mabadiliko ya kidemokrasia na kukubalika kwa chama hicho visiwani humo Lowassa ametoa wito kwa wanachama na viongozi wa chama hicho kuiondolea uvivu CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!