June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ligi Kuu Bara kuanza rasmi Septemba 29

Spread the love

 

LIGI Kuu soka Tanzania Bara kwa msimu wa 2021/22, itaanza kupigwa kuanzia tarehe 29 Septemba 2021, mara baada ya kuchezwa mchezo wa ngao ya hisani kati ya Simba na Yanga. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa ngao utapigwa tarehe 25, Septemba 2021, kwenye dimba la Benjamin Mkapa, majira ya saa 11 jioni.

Akizungumza hii leo mara baada ya kikao na Wenyeviti wa klabu za Ligi Kuu, mtendaji Mkuu wa bodi ya Ligi Almas Kasongo Ligi hiyo itaanza tarehe 29, mara baada ya kupitisha baadhi ya kanuni.

“Kwa mujibu wa kalenda yetu kuelekea msimu ujao, tarehe 25 tutaufungua msimu wetu rasmi kwa mchezo wa ngao wa hisani kati ya Simba na Yanga.”

Almas Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB)

“Baada ya hiyo mechi tutakuwa na mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi Kuu ambao utakuwa tarehe 29.”Alisema Kasongo

Katika hatua nyingine mtendaji huyo Mkuu alisema kuwa, ratiba ya Ligi hiyo itatoka hivi karibuni, ili klabu zianze maandalizi mapema.

“Baada ya siku mbili hizi tutatoa ratiba yenye ukamilifu wake ili timu zifanye maandalizi.”

error: Content is protected !!