Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Michezo Peter Banda afungua usajili Simba
MichezoTangulizi

Peter Banda afungua usajili Simba

Spread the love

 

Winga wa kimataifa wa Malawi Peter Banda, amekuwa mchezaji wa kwanza kufungua dirisha la usajilin ndani ya klabu ya Simba mara baada ya kutambulisha hii leo kama mchezaji mpya ndani ya kikosi hiko. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Usajili wa kinda hilo (20), umekuwa wa kwanza ndani ya klabu hiyo toka kufunguliwa kwa dirisha la usajili tarehe 19 Julai 2021.

Mchezaji huyo ambaye anamilikiwa na klabu ya Nyasa Bullets ya nchini Malawi, amejiunga na Simba akitokea kwenye klabu ya Sherrif FC ambapo alipokuwa akicheza kwa mkopo na mkataba wake kumalizika.

Kusajiliwa kwa winga huyo, huwenda kukawa mwisho wa nyota kutoka nchini Zimbabwe Perfect Chikwende ambaye alisajiliwa kwenye dirisha dogo na kushindwa kuonesha makali yake.

Mchezaji huyo amejiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu kewa mkataba wa miaka mitatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!