June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Manara: Umarufu na Biashara zimeniondoa Simba

Haji Manara

Spread the love

 

 ALIYEKUWA Afisa Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa sababu za kufanya biashara na kampuni zingine na umaarufu alioputa ndani ya klabu hiyo ndio zimemuondoa ndani ya Simba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Manara ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa Habari, uliofanyika jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwashukuru wanasimba mara baada ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo na kuteuliwa Ezekiel Kamwaga.

Afisa habari huyo wa zamani aliukataa mkabata aliopewa na klabu hiyo wenye thamani ya shilingi 3 milioni, kwa ulikuwa na kipengele kilichokuwa kinambana kutangaza bidhaa nyingine.

“Mkataba wa kwanza niliopewa nikaukataa kwa kuwa ulikuwa na kipengele cha kutofanya kazi na kampuni yoyote zaidi ya Mohammed Enterprises na ulikuwa Mil 3.”

Barbara Gonzalez, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba

“Alivyondoka Senzo nikaanza mkataba na Azam TV, kwa kunipa ofa ya kutangaza bidhaa zao, nikaanza nikiona nikipost Maji ya Uhai nikaona bwana mkubwa anaposti kunywa maji ya Masafi, uvumilivu ukanishinda nikamuambia.” Alisema Haji Manara

Manara aliingia Simba mwaka 2015 na kuhudumu katika nafasi ya usemaji katika kipindi cha miaka sita, huku akifunguka kuwa katika kipindi chote hakuwa na mkataba.

Mohamed Dewji (MO), Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Simba

Nafasi ya sasa ya Haji Manara ndani ya klabu ya Simba inashikiliwa na Ezekiel Kamwaga, ambaye atakaimu kiti hiko kwa muda wa miezi miwili kabla ya kutangaza nafasi za kazi.

error: Content is protected !!