MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana, amesema vyama vya siasa vinampongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa namna anavyoongoza nchi, pamoja na kuimarisha umoja wa kitaifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).
Kinana ametoa kauli hiyo leo tarehe 31 Agosti 2023, akizungumza katika hafla ya kufunga Tamasha la Kizimkazi, visiwani Zanzibar.
“Nataka niseme sisi wana CCM tunajivunia uongozi wako na nina hakika mimi binafsi nina mazungumzo mara kadhaa na vyama vingine, hata juzi tulikaa siku tatu na vyama vyote katika Baraza la Vyama vya Siasa, kila chama kiliposimama, kilipongeza kwa namna unavyoiongoza nchi, ulivyoleta maridhiano na ulivyoimarisha umoja wa taifa letu,” amesema Kinana.
Kuhusu tamasha hilo, Kinana amezitaka mamlaka zinazoandaa kuhakikisha wanaliboresha ili lipate umaarufu nje ya Tanzania kwa ajili ya kuvutia watalii.
Leave a comment