Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kinana akemea ukanda, ukabila CCM
Habari za SiasaTangulizi

Kinana akemea ukanda, ukabila CCM

Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM
Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amekemea vitendo vya ukabila, udini na ukanda, ndani ya chama hicho, akisema hakuna anayekimiliki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kinana ametoa kauli hiyo leo Ijumaa, tarehe 1 Aprili 2022, muda mfupi baada ya kupitishwa kushika wadhifa huo, kwa asilimia 100 ya kura za wajumbe 1,875 wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, uliofanyika jijini Dodoma.

“Hiki chama ni kikubwa, kina wanachama wengi sana, kuna watu sio wanachama lakini wanakipenda sana. Nataka niwasihi hakuna chama cha mtu, kuna Chama Cha Mapinduzi, ndani ya chama hiki hakuna ukanda,” amesema Kinana.

Kinana amesema “mara nyingi Mzee Joseph Warioba anapenda kututahadharisha haya mambo ya ukanda na udini tukae nayo mbali na katika kufanya kazi nitajitahidi kupambana na hayo mambo. Mtu akikosa kukubalika anaingia kwenye kichaka cha ukanda, ukabila na udini si sawa kwa chama hiki.”

Katika hatua nyingine, Kinana amewataka wanachama wa CCM, kutoisema vibaya Serikali hadharani pindi panapokuwa na kasoro, bali wapeleke malalamiko yao ndani ya vikao vya chama hicho.

“Si sawa kwa mwanaCCM kwenda hadharani kuisema Serikali yake vibaya, lakini Serikali ina wajibu wa kuisimamia Serikali na leo nimesoma marekebisho ya katiba inasema kila miezi sita kutakuwa na vikao vya chama vya kutathimini Ilani ya CCM na hapo ndipo pa kuzungumza,” amesema Kinana.

Kinana amewataka wanachama wa CCM, kuwa mstari wa mbele katika kueleza kwa umma utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho 2020-2025.

“Pale Serikali inapokuwa na kasoro, utekelezaji unapokuwa na mapungufu wana CCM tuna wajibu wa kuzisemea. Kuwasemea wananchi kuhusu kasoro na hizo kasoro tusiziseme kwa kufoka au kwa kejeli,” amesema Kinana.

Kinana amepitishwa na CCM kuwa Makamu Mwenyekiti wake Bara, kufuatia kung’atuka kwa aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo, Mzee Phillip Mangula.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!