Thursday , 13 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kikwete amuwakilisha Samia mazishi ya Rais Finland
Habari za Siasa

Kikwete amuwakilisha Samia mazishi ya Rais Finland

Spread the love

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya Mazishi ya Kitaifa ya Rais wa zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari iliyofanyika Helsinki tarehe 10 Novemba 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akitoa salamu za pole, Rais Kikwete alisema kuwa Rais Samia ametoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Findland, Sauli Niinistö, Familia ya Marehemu na watu wote wa Finland kufuatia kifo cha kiongozi huyo mkubwa duniani.

Rais Kikwete aliungana na viongozi mbalimbali walioshiriki mazishi hayo wakimwemo Rais wa Kosovo, Vyosa Osmani na Rais wa Namibia, Hage Geingob na kummwagia sifa Hayati Martti Ahtisaari kwamba alikuwa kiongozi mwenye maono na mpenda amani duniani.

Hayati Martti Ahtisaari aliwahi kuwa Balozi wa Finland nchini Tanzania kuanzia mwaka 1973 hadi 1976 na alikuwa Rais wa Finland kuanzia mwaka 1994 hadi 2000.

Katika vipndi vyote hivyo, Hayati Martti Ahtisaari aliimarisha uhusiano wa Tanzania na Finland katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania mwaka 1997 wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu iliyokuwa inaongozwa na Hayati Benjamin Mkapa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Prof. Mkumbo: Pato la taifa limefikia trilioni 148

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema mwaka...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Deni la Serikali lafikia trilioni 91

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mbunge Dk. Shogo Mlozi afariki dunia

Spread the loveMbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambaye pia ni...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Marekani yasaka fursa uwekezaji sekta ya nishati Tanzania

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amekutana...

error: Content is protected !!