Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Kikwete ahoji wanaume wamekwenda wapi
Elimu

Kikwete ahoji wanaume wamekwenda wapi

Jakaya Kikwete, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Spread the love

 

MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Jakaya Kikwete, ametaka utafiti ufanyike ili kujua kwa nini idadi ya wanaume katika kujiunga na taaluma kwenye chuo hicho imepungua, kwa kuwa katika udahili wake wa 2022 wanawake wameongezeka na kufikia asilimia 53. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Kikwete ambaye ni Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, ametoa kauli hiyo leo Jumatano, tarehe 30 Novemba 2022, katika mahafali ya 52 ya duru ya tano ya UDSM, baada ya Makamu Mkuu wa UDSM anayeshughulikia Taaluma, Prof. Boniventure Rutinwa, kusema wanafunzi 313 kati ya 640 (50%), wlaiopata ufadhili wa masomo kutoka Ufadhili wa Rais Samia Suluhu Hassan, wamejiunga na chuo hicho.

“Tuseme katika udahili mwaka huu asilimia 53 ni wanawake, sasa sijui watoto wa kiume wamekwenda wapi siku hizi, itabidi suala hili tukae na kulifanyia utafiuti huko waliokwenda sijui ni wapi,” amesema Dk. Kikwete.

Aidha, Dk. Kikwete ameponegza kitendo cha ongezeko la wanawake kujiunga chuoni hapo tena katika masomo ya sayansi, akisema huko nyuma ushiriki wao katika taaluma ulikuwa mdogo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

ElimuMakala & Uchambuzi

Waraka maalumu kwa NECTA, “hawapaswi kuungwa mkono”

Spread the loveHATUA iliyotangazwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), ya...

Elimu

NACTVET yafungua dirisha la udahili

Spread the love  BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo...

Elimu

Prof. Mwakalila awafunda wanafunzi Chuo Mwalimu Nyerere, “ulipaji ada ni muhimu”

Spread the love  MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere (MNMA),...

error: Content is protected !!