Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Kikwete ataka utafiti uchache wa wanaume kujiunga UDSM
Elimu

Kikwete ataka utafiti uchache wa wanaume kujiunga UDSM

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
Spread the love

 

MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Jakaya Kikwete ametaka utafiti ufanyike ili kujua kwa nini idadi ya wanaume katika kujiunga na taaluma kwenye chuo hicho imepungua, kwa kuwa katika udahili wake wa 2022 wanawake wameongezeka na kufikia asilimia 53. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Kikwete ambaye ni Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, ametoa kauli hiyo leo Jumatano, tarehe 30 Novemba 2022, katika mahafali ya 52 ya duru ya tano ya UDSM.

Ni baada ya Makamu Mkuu wa UDSM anayeshughulikia Taaluma, Prof. Boniventure Rutinwa, kusema kuwa wanafunzi 313 kati ya 640 (50%), waliopata ufadhili wa masomo kutoka Ufadhili wa Rais Samia Suluhu Hassan, wamejiunga na chuo hicho.

“Tuseme katika udahili mwaka huu asilimia 53 ni wanawake, sasa sijui watoto wa kiume wamekwenda wapi siku hizi, itabidi suala hili tukae na kulifanyia utafiuti huko waliokwenda sijui ni wapi,” amesema Dk. Kikwete.

Aidha, Dk. Kikwete amepongeza kitendo cha ongezeko la wanawake kujiunga chuoni hapo tena katika masomo ya sayansi, akisema huko nyuma ushiriki wao katika taaluma ulikuwa mdogo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

RC Songwe ang’aka kesi 2 kati ya 60 za mafataki kuamuliwa

Spread the loveMkuu wa mkoa wa Songwe Dk. Fransis Michael ameshangazwa na...

error: Content is protected !!