ALIYEKUWA Rais wa China, Jiang Zemin, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96 kutokana na matatizo ya saratani ya damu na baadhi ya viungo vyake vya mwili kushindwa kufanya kazi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Taarifa ya kifo hicho imetangazwa na Serikali ya China, ambapo kwa mujibu wa Shirika la Habari la taifa hilo, Zemin amefariki dunia Jumatano, tarehe 30 Novemba 2022.
Zemin alikuwa Rais wa China, kuanzia 1993 hadi 2003.
Zemin alihudumu katika nyadhifa mbalimbali nchini China, ikiwemo nafasi ya katibu mkuu wa Chama cha Kikumonusti cha China, kuanzia 1989 hadi 2022.
Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, kiongozi huyo mstaafu wa China, kabla ya kukutwa na umauti kwa mara ya mwisho alionekana hadharani 2019.
Leave a comment