Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kigogo ACT-Wazalendo: Vyama vya upinzani vilikosea kumpokea Membe, Lowassa
Habari za Siasa

Kigogo ACT-Wazalendo: Vyama vya upinzani vilikosea kumpokea Membe, Lowassa

Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo
Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amesema vyama vya upinzani vilifanya makosa kuwapokea baadhi ya makada waliotoka katika chama tawala cha CCM, kisha kuwapa dhamana ya kugombea nafasi za uongozi katika chaguzi mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Ado ametoa kauli hiyo leo tarehe 2 Februari 2023, akihojiwa na Kituo cha Redio cha East Africa.

Mwanasiasa huyo amedai kuwa, baadhi ya wanachama hao baada ya muda hurejea CCM, ambapo amemtolea mfano Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, aliyehamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kupewa ridhaa ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Pamoja na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, aliyepokewa na chama chake kisha kumteua kugombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, ambao wote katika nyakati tofauti walirejea CCM.

“Uzoefu unaonyesha wenzetu kutoka CCM kama wataondoka kwa tofauti zao baada ya muda kwa kauli yake yeye mwenyewe Mzee Membe, anasema wanakumbuka nyumbani maana yake anasema niliwa-miss sana nyumbani, sasa hilo ni funzo. Uchambuzi wangu ni kwamba Lowassa na Membe yalikuwa makosa ya vyama vya upinzani,” amesema Ado.

Katika hatua nyingine, Ado amevitaka vyama vya siasa vya upinzani kuandaa wanachama wake kushika nafasi nyeti za uongozi ikiwemo Urais, kama ACT-Wazalendo inavyofanya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.

“Siasa ni mapambano ya hoja na ACT Wazalendo ndio Chama kinachokuwa kwa kasi nchini hivi sasa ukizungumzia vyama vitatu vikubwa vya siasa huwezi kuikosa ACT kwahiyo inapokuwa kwa kasi inatishia nafasi za watu na inazalisha minyukano,” amesema Ado.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!