Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 
Habari Mchanganyiko

Kasilda Mgeni anasisitiza umoja, ushirikiano Same 

Mkuu mpya wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni akikabidhiwa nyaraka za ofisi na Mkuu wa Wilaya hiyo aliyehamishwa wilayani Ilala, Edward Mpogolo
Spread the love

 

MKUU mpya wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewaomba watumishi wa umma wilayani hapo kudumisha umoja na ushirikiano ili kuchochea maendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Same … (endelea).    

Mgeni amesema hayo wakati akizungumza na wakuu wa idara pamoja na taasisi mbalimbali  Wilaya ya Same  mara baada ya kupokelewa.

DC Mgeni ametoa shukrani za dhati kwa wakuu wa   idara kwa mapokezi makubwa ambayo amekutana nayo na kuahidi kushirikiana nao ili kuipaisha Same katika sekta za kijamii, kiuchumi na maendeleo.

Amesema mapokezi hayo hakuyatarajia na kusema hii inaonesha mshikamo mkubwa uliopo kwa viongozi hao katika uwajibikaji wa kazi 

Aliendelea kusema na kuwaomba wakuu wa idara zote kuendelea kushirikiana kwa pamoja lengo ni mkusaidia Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwatumikia wananchi na kusimamia miradi  yote ambayo inayoendelea  kwenye wilaya hiyo.

Kwa upande wake aliyekuwa DC wa Same, Edward Mpogolo amewaomba wakuu wa idara zote kumpa ushirikiano wa kutosha mkuu wa wilaya mpya na kuonyesha uzalendo kwa Taifa na wananchi kwa ujumla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!