June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Karia, Kidao wachanjwa

Walace Karia, Rais wa TFF

Spread the love

 

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia ni miongoni mwa viuongozi waliopata chanjo ya corona, katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Da es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu….(endelea)

Uzinduzi wa chanjo huo, ulifanyika jana Ikulu jijini Dar es Salaam na zoezi la kupata chanjo hiyo, liliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia Suluhu Hassan akichanjwa chanjo ya korona

Katika taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo, hii leo imeeleza kuwa, Rais Karia ametoa rai kwa wanamichezo nchini, kuchanja mara baada ya Serikali itakapotoa utaratibu.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, (TFF) Wilfred Kidao

Rais Karia hakuwa peke yake kwenye zoezi hilo, aliongozana na Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, Athuman Nyamlani pamoja na katibu Mkuu Wilfred Kidao.

 

 

 

 

error: Content is protected !!