Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari Karagwe watenga bilioni 1.32 kupokea wanafunzi wapya 2023
HabariHabari Mchanganyiko

Karagwe watenga bilioni 1.32 kupokea wanafunzi wapya 2023

Spread the love

HALMASHAURI ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera inatarajiwa kutumia Sh bilioni 1.32 katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 66 kwa mwaka huu wa fedha ili kuanza maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.

Pia fedha hizo zitakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali za sekondari pamoja na majengo katika Hospitali ya Wilaya ya Karagwe. Anaripoti Paul Kayanda, Kagera … (endelea)

Hayo yamebainisha na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Michael Nzyungu alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari ofisini tarehe 8 Disemba, 2022.

Amefafanua kuwa shule mojawapo iliyopewa fedha ni shule ya Sekondari Rugu iliyopo kitongoji cha Nyakahanga kijiji cha Rugu wilayani humo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.

Amesema kuwa madarasa yote 66 yapo kwenye hatua mbalimbali za kuezeka na umaliziaji na hatimaye baada ya muda mfupi madarasa yote yatakuwa yamekamilika kwa halmashauri nzima.

“Tunamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha hizo na kwamba fedha hizi zimeletwa kwa awamu nne awamu ya kwanza Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kwa yale majengo waliyoelekezwa Halmashauri iliongeza kiasi cha shilingi milioni 300.

Muonekano wa Jengo la wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospital ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera.

“Kwa hiyo awamu ya kwanza ina majengo saba, Jengo la Utawala, OPD, Maabara, x-ray, Wodi ya wazazi pamoja na mambo mengine ambayo yalitumia kiasi cha Sh bilioni 1.8 na bilioni1.5 zilikuwa za serikali kuu na Halmashauri ikatoa milioni 300, hiyo ilikuwa ni awamu ya kwanza 2001,” amesema Nzyungu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!