Sunday , 19 May 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Kampuni ya Shanta Gold Mine inavyounga mkono Serikali kwa huduma za jamii
Makala & Uchambuzi

Kampuni ya Shanta Gold Mine inavyounga mkono Serikali kwa huduma za jamii

Spread the love

 

KAMPUNI ya uchimbaji wa dhahabu Shanta Gold Mine kupitia mgodi wake wa New Luika iliyoko kata ya Mbangala wilayani Songwe mkoani hapa imetumia zaidi ya Sh 150 milioni katika ujenzi wa miradi ya maji, nyumba za walimu na ujenzi wa barabara ya kiwango cha changarawe ikiunga jitihada za serikali katika utatuzi wa changamoto za wananchi. Anaandika Ibrahim Yassin … (endelea).

Changamoto kubwa iliyokuwepo kwa wakazi wa wilaya hiyo ni ukosefu wa maji safi na salama hali iliyosababisha uwepo wa homa za kipindupindu kwa nyakati kadhaa huku ukosefu wa nyumba za walimu ukisababisha baadhi ya walimu kugoma kwenda kufundisha shule za vijijini kutokana.

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada kubwa kwa kutoa kiasi cha Sh 1.5 Bilioni katika kila halmashauri kujenga barabara za viwango vya lami kiwango cha kati katika barabara za zinazozunguka miji pia kwa mkoa wa Songwe imetoa Sh 20.5 Bilioni kujenga miradi ya maji.

Ukiachana na fedha hizo pia serikali imetoa zaidi ya Sh 1 Bilion kwa mkoa wa Songwe kujenga madarasa shinikizi kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza ambapo wanafunzi wattaweza kusoma wakiwa darasani na wakikalia madawati ukilinganisha na ilivyokuwa awali ambapo wanafunzi walisoma kwa kupokezana.

Kampuni ya Shanta Gold Mine imeunga juhudi za serikali kwa kujenga barabara kutoka barabara kuu ikwenda kwenye vitongozi vilivyopo kata ya Mbangala na ujenzi upo asilimia 75 ambapo awali wananchi walipata changamoto ya kutumia njia ya mzunguko kwenda makao makuu ya wilaya hali iliyohatarisha maisha yao.

Pia kampuni hiyo imeweza kutumia Sh 89 Milioni kujenga nyumba za walimu ambapo pia imetumia sh 84 milioni kujenga mradi wa maji wakitumia chanzo cha Mto Luika uliopo kilometa 4 na sasa wakazi wa kijiji cha Mbangala na majirani zao wanatumia maji safi na salama na uondokanana adha ya kutembea umbali mrefu kufuata majji.

Meneja wa kampuni hiyo, Mahandisi Exupery Lyimo anasema wamefanya hivyo wakifuata sheria inavyotaka kwani kampuni ipo kwenye kata ya Mbangala hivyominapaswa kusaidia katika ujenzi wa miradi inayogusa jamii kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi.

Lyimo,anasema,katika mwaka 2021 kampuni hiyo ya Shanta ilitumia kiasi cha Sh 478 milioni katika ujenzi wa miradi na michango mbalimbali ya maendeleo kwa wilaya ya Songwe,na kwamba makisio ya bajeti ya mwaka 2022 ni Sh 723 Milioni na kwa mwaka 2023 ni Sh 779 milioni.

Anasema mbali na kampuni hii inaunga mkono jitihada za serikali katika ujenzi wa miradi inayogusa jamii wanaikabidhi miradi hiyo kwa wenyekiti wa halmashauri na itazinduliwa na Mbunge,pia wanawaomba wanakijiji wanaoishi karibu na miradi hiyo kwamba kila mmoja ahusike katika kuilinda miradi hiyo ili iweze kuwasaidia wao na vizazi vijavyo.

MWENYEKITI WA HALMASHAURI NA MBUNGE WA JIMBO BAADA YA KUKABIDHIWA MIRADI WATOA NENO.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo,Abraham Sambila,baada ya kukabidhiwa miradi hiyo,anasema wanafuraha kubwa kukabidhiwa miradi mitatu kwa wakati mmoja,nyumba ya walimu ujenzi wa barabara na mradi wa maji.

Anasema kwa mradi wa maji wananchi na hata wanafunzi walitembea kilometa 4 hadi mto Luika kusaka maji walipoteza muda wa kujisomea na wazazi walipoteza muda wa kufanya shughuri zingine za uzalishaji mali hivyo kwa sasa anaamini elimu itapaa na wazazi wataongezea uchumi wao kwa kufanya kazi zingine.

‘’Kawaida kila mradi wa muwekezaji ukiwepo eneo furani ni wajibu wa kisheria kujenga miradi ya maendeleo kwa wanakijiji wanaozunguka mradi ambapo sheria ya CSR inamvyomtaka muwekezji wa madini atoe asilimia kadhaa ya kipato kusaidia jamii,lakini kampuni hiyo imeenda mbali zaidi imeweza kuvisaidia vijiji hata vya mbali.

Mbunge wa jimbo la Songwe Phlipo Mulugo,anasema anakila sababu ya kuipongeza kampuni hiyo,kwa kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo muhimu ambayo lea ameweza kuizindua kwa ajili ya kuanza kutumika na kwamba kwa sasa wanatembea kifua mbele wakijivunia maendeleo yaliyopo jimboni humo.

Alisema licha ya kuwa katika maeneo hayo kuna miradi ya Kiserikali inayoendelea kujengwa lakini kampuni pia imeunga jitihada hizo kwa kujenga miradi hiyo,na kwamba umuhimu wa barabara hiyo itakuza uchumi wa wananchi kwani mita 40 kutoka hapo kuna ziwa Rukwa na wavuvi wataituia barabara hiyo kusafirisha samaki.

‘’Tunaipongeza kampuni ya shanta kwa miradi hiyo mitatu,kazi iliyopo kwa wananchi ni kuitunza na kuwawajibisha watakaokao haribu miradi,wazee wa mila (Mamwene) nawaomba muwe wakali kwa watu watakaobainika wanaharibu miradi,serikali na wadau wamefanya kazi kubwa kilichobaki ni kuitunza ili isiharibiwe’’anasema Mulugo.

Akimuwakilisha Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Lucian Yunga,anasema kampuni imefanya kazi kubwa anaamini kiwango cha ufaulu kitaongezeka kwani muda wa wanafunzi waliokuwa wakiutumia kusaka maji kilometa 4 watautumia kusoma,mkuu wa shule na viongozi wa vijiji wanapaswa kuhakikisha wanaisimamia miradi hiyo ili isiharibiwe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Potofu huzaa potoshi/ potoshi huzaa potofu?

Spread the loveDayosisi 7 za KKKT katika kanda ya Ziwa na Magharibi,...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

error: Content is protected !!