Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu atinga Polisi kuchukua gari lake “nataka nilipeleke makumbusho”
Habari za SiasaTangulizi

Lissu atinga Polisi kuchukua gari lake “nataka nilipeleke makumbusho”

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ametinga katika Ofisi ya Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, kufuata gari lake alilokuwemo wakati anashambuliwa risasi na watu wasiojulikana tarehe 7 Septemba 2017. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Lissu amefika katika ofisi hizo leo Alhamisi, tarehe 9 Februari 2023, baada ya kuwasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Martin Otieno, lakini hakufanikiwa kutokana na kiongozi huyo wa Polisi kuwa nje ya ofisi kwa ajili ya majukumu mengine.

Baada ya kufika katika ofisi hizo, Lissu alipokelewa na baadhi ya maafisa wa Polisi, ambapo mmoja wao alimueleza kwamba Kamanda Otieno yuko nje ya ofisi akifuatilia ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo mkoani humo na kupoteza maisha ya watu 12.

Lissu alielekezwa arudi katika ofisi hizo wakati mwingine ambapo Kamanda Otieno atakuwa amerejea. Hata hivyo, mwanasiasa huyo alihoji kama anaweza ruhusiwa kuliona ambapo alijibiwa kwamba, anapaswa asubiri hadi kamanda huyo atakapokuwa ofisini.

Akizungumza na wanahabari muda mfupi baada ya kupewa taarifa hiyo, Lissu amedai kwamba aliwasiliana na Kamanda Otieno wakati akiwa njiani kutoka Singida, akimtaka wazungumze juu ya namna gani atakavyopata gari lake lililoshikiliwa na Jeshi la Polisi, kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la kushambuliwa risasi na watu wasiojulikana.

Lissu amesema kuwa, analitaka gari lake alitumie au alipeleke katika makumbusho ambayo hakuyataja jina.

“Tangu tarehe 7 Septemba 2017 hadi leo gari imekuwa mikononi mwa Polisi na mimi sijawahi kuiona, nilikuja tuzungumze na RPC wanioneshe niione ilivyoharibiwa, halafu tuzungumze utaratibu wa namna ya kurudishiwa gari langu sababu nahitaji kuitumia au pengine kuipeleka makumbusho,” amesema Lissu na kuongeza:

“RPC aliniambia kuna ajali imetokea Kongwa akaniambia anatoka huko akifika nije tuonane naye, wala hakuna zengwe.”

Lissu amefika Dodoma, ikiwa zimepita siku kadhaa baada ya kuwasili Tanzania akitokea Ubelgiji, alikokimbilia baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa 2020, ambapo alidai aliamua kurejea kuishi ughaibu kunusuru maisha yake baada ya kupokea vitisho vya kiusalama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

error: Content is protected !!