Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Jua kupatwa leo Aprili 8, 2024, TMA yatoa elimu, Tanzania haitashuhudia
Habari Mchanganyiko

Jua kupatwa leo Aprili 8, 2024, TMA yatoa elimu, Tanzania haitashuhudia

Spread the love

MAMLAKA ya Hali Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya hali ya kupatwa kwa jua tukio linalohusisha kivuli cha mwezi kuangukia juu ya uso wa Dunia ambapo katika maeneo yaliyo ndani ya kivuli hicho jua huonekana likifunikwa na Mwezi kwa kipindi cha saa chache. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa ya TMA, imesema kuwa kuna aina mbili za kupatwa kwa Jua; kupatwa kwa jua kikamilifu ambapo mwezi huzuia kabisa mwanga wa jua kufika katika Dunia na aina ya pili, kupatwa kwa Jua Kipete, Mwezi huzuia sehemu tu ya mwanga wa Jua, hivyo kutengeneza umbo la pete ya mwanga wa jua angani.

Jumatatu ya Aprili 8, 2024, kunatarajiwa kutokea kwa tukio la kupatwa kwa Jua Kikamilifu. Tukio hili linatarajiwa kutokea upande wa Bara la Amerika ya Kaskazini kupitia Mexico, Marekani na Canada.

Aidha, tukio hili linatarajiwa kuanzia maeneo ya kusini mwa Bahari ya Pasifiki ambapo Mexico itakuwa nchi ya kwanza kufikiwa na kupatwa kwa jua kikamilifu mnamo majira ya saa 5:07 asubuhi kwa saa za Amerika.

Njia ya kupatwa kwa Jua itaendelea kutokea Mexico na kuingia Texas, Marekani majira ya saa 7:40 mchana ikipita baadhi ya maeneo na kisha kuingia Kusini mwa Ontario, Canada na kutoka Bara la Amerika ya Kaskazini kupitia pwani ya Bahari ya Atlantiki katika mji wa Newfoundland, Kanada, saa 11:16 jioni.

Kwa kawaida, sehemu ya jua inayofunikwa na mwezi wakati wa kilele cha kupatwa kwa jua kikamilifu itatofautiana baina ya eneo na eneo.

Maeneo yaliyo ndani ya njia ya kupatwa kwa jua kikamilifu yataona kupatwa kwa Jua kwa kiwango kikubwa zaidi ikilinganishwa na maeneo yaliyo mbali zaidi na njia hii.

Kwa kuwa Tanzania inaangukia katika eneo la mbali zaidi na njia hiyo, hivyo haitashuhudia tukio hilo. Aidha, kutokana na tukio hili kutokea mbali zaidi na nchi yetu, athari za moja kwa moja katika masuala ya kijamii na kiuchumi hazitarajiwi kuonekana hapa nchini.

Mamlaka ya hali ya hewa inaendelea kufuatilia na itatoa taarifa za mabadiliko yoyote yanayoweza kujitokeza katika hali ya hewa kulingana na tukio hili la kupatwa kwa jua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!