Saturday , 15 June 2024
KimataifaTangulizi

Jammeh anyosha mikono

Yahya Jammeh, Rais wa Gambia aliyeangushwa katika uchaguzi Mkuu
Spread the love

HATIMAYE Yahya Jammeh, Rais wa Gambia aliyetaka kubaki Ikulu kwa hila ametangaza kuachia madaraka bila shuruti, anaandika Wolfram Mwalongo.

Jammeh ametangazia umma kwa njia ya televishehi kwamba, hatothubutu kuona damu ikimwagika katika taifa lake taarifa ambazo zimepokelewa kwa furaha na maelfu ya raia nchini mwake.

Hatua hiyo imefuatia jitihada za marais wawili Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania na Alpha Conde wa Guinea kusitisha jeshi la Jumuhiya ya Kiuchumi Afrika Magharibi (ECOWAS) ambalo lilimpa muda wa ziada na baada ya hapo angeondolewa kwa mtutu.

Marais hao waliweza kuingia Banjul Mji, Mkuu wa Gambia na kufanikiwa kuingia Ikulu ya nchi hiyo ambapo waliweza kumshawishi na na baadaye kutangaza mwenye (Jammeh) kwamba ataachia mamulaka.

“Nimeamua leo, nikiwa na dhamiri njema, kuachia uongozi wa taifa hili kubwa nikiwa na shukrani zisizo na kikomo kwa raia wa Gambia.

“Namuahidi Allah na taifa lote kwamba masuala ambayo yanatukabili kwa sasa yatatauliwa kwa njia ya amani,”amesema Jammeh.

Hata hivyo Rais Jammeh anapaswa kuondoka nchini humo hiyo ni kwa mujibu wa maafikiano waliyofikia na kiongozi huyo aliye ishi Ikulu kwa miaka 22 sasa.

Mtando wa wa Habari wa Concise wa nchini Nigeria umeeleza Rais Jammeh ataondoka nchini Gambia wakati wowote, kumpisha Adama Barrow, rais mpya aliyeapishwa ubalozini nchini Senegal.

Rais Jammeh kama angeliendelea na msimamo wake Jeshi la ECOWAS linalo ongozwa na Jashi la Nigeria tayari lilisha weka nanga katika Ardhi ya Gambia, Jambo linalotajwa kuzidisha hofu kwa Wagambia huku wengine wakikimbilia uhamishoni nchi jirani a Senegal.

Ambapo kwamjibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi duniani la nchini Senegal limethibitisha kupokea zais ya Wagambia 100,000 walikimbia nchi kwa kuhofu ya machafuko.

Aidha, viongozi wa Serikali hususani Mawaziri waliojiuzulu kwenye Serikali ya kwa nguvuwanaRipotiwa Kulikimbia taifa lao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Samia: Wakuu wa mikoa, wilaya wanaendeleza ubabe

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema bado wakuu wa wilaya na...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

Habari za SiasaTangulizi

Gesi asilia, petroli kodi juu

Spread the loveWaziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza kufanya marekebisho kwenye...

error: Content is protected !!