August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jammeh apagawa, atimua mawaziri

Rais Yahya Jammeh anayeikalia Gambia kwa mabavu

Spread the love

WAKATI muda wa Yahya jammeh rais ‘king’ang’anizi’ wa Gambia ukiwa umeisha na hatua za kumuondoa kwa nguvu zikisubiriwa kuanza, kiongozi huyo amevunja rasmi Baraza la Mawaziri, anaandika Wolfram Mwalongo.

Shirika la habari la Uingereza (BBC) limeripoti kwamba kujiuzulu kwa mawaziri saba, pamoja na Isatou Njie aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jammeh kumemfanya Jammeh kuvunja baraza lake.

Idadi ya watendaji wanaojiweka kando na rais huyo imemuongezea hofu zaidi wakati vyombo vya usalama vikigawanyika pande mbili -wanaomuunga mkono Rais Jammeh dhidi ya wanaoafiki utawala mpya wa Rais Adama Barrow aliyeapishwa akiwa uhamishoni nchini Senegal.

error: Content is protected !!