Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CUF, Chadema wagawa kura
Habari za SiasaTangulizi

CUF, Chadema wagawa kura

Edward Lowassa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema (kulia) akiteta jambo na Maalim Seif Sharrif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF
Spread the love

ATHARI ya mtifuano ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) zinaendelea ambapo sasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinawinda kura za CUF, anaandika Christina Haule.

Chadema mkoani Morogoro kimeomba wanachama wa CUF wanaounga mkono chama hicho kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Kiwanja cha Ndege kukipa kura Chadema.

Hatua hiyo inakuja baada ya Chadema kudai kwamba, mgombea wa CUF kwenye kata hiyo Mlapokolo anahujumu Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa kuungana na Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Prof. Lipumba amekuwa akizunguka kwenye kata mbalimbali za uchaguzi Tanzania Bara kuwanadi wagombea wa udiwani kwenye uchaguzi mdogo unaotarajia kufanyika kesho.

Kiongozi huyo wa CUF amekuwa akizunguka na wale wanaomuunga mkondo ndani ya chama hicho kilichopasuka vipende viwili kutokana na mgogoro wa kiuongozi unaotawala kwa sasa.

Miongoni mwa viongozi wanaomuunga mkono Prof. Lipumba ni pamoja na Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Abdul Kambaya, Naibu Mkurugrnzi wa Mawasiliano na Umma wa chama hicho.

Chadema katika Kata ya Kiwanja cha Ndege, Morogoro kikimnadi mgombea wake Salum Milindi kimedai kuwa, Mlapakolo anauza utu wake kwa kumuunga mkono Prof. Lipumba na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kauli hiyo imetolewa na Matwew Mlipina, Kiongozi wa Chadema Makao Makuu ya chama hicho Morogoro jana na kwamba, Mlapakola ni mamluki.

Mlipina amedai kwamba, Prof. Lipumba ni mamluki wa CCM tangu mwaka 1992 baada ya kusababisha kuvunjika kwa kamati kwenye kikao cha kujadili katiba wakati akigombania fedha.

Na kwamba, ili Mlapakolo alinde heshima yake anapaswa kujitoa huko kwanza kwa kuwa, wakati huu haeleweki kwa wananchi.

Hivyo aliwaomba wanachama wa CUF kuwa na uamuzi sahihi na kumchagua Milindi ili aweze kuwaongoza sababu ana nguvu, nia na uwezo wa kuwasaidia na kuleta maendeleo kwa wanakiwanja cha ndege.

Elisa Ninja, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati |(Morogoro, Dodoma  na Singida) amewasihi wakazi wa kata hiyo kumchagua mgombea wao katika uchaguzi huo ili kuweza kupata maendeleo ya kweli.

Hata hivyo, ameliomba Jeshi la Polisi nchini, kuona umuhimu wa kufanya kazi yao bila upendeleo kwa kutatua sawa matatizo na migogoro ya kisiasa yanayojitokeza kuanzia ngazi ya kata hadi Taifa.

Mgombea wa udiwani kata hiyo Milindi amewaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua na kuwa kiongozi wao huku akiahidi kutatua kero mbalimbali zilizopo kwenye kata hiyo na kuwaletea maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!